Kuhusu ruhusa za WhatsApp

Android
iPhone
Unapotumia vipengele kwenye WhatsApp kwa mara ya kwanza, WhatsApp inaweza kuhitaji idhini ya kufikia maelezo au programu kwenye iPhone yako. Kuzima kipengele cha ruhusa kunaweza kusababisha WhatsApp ipoteze utendaji fulani.
Ikiwa tayari umesakinisha WhatsApp, unaweza kudhibiti ruhusa ambazo programu inatumia kwenye mipangilio ya simu yako. Unaweza kuangalia mipangilio ya ufikiaji wa iPhone yako kwa kufuata hatua hizi:
  1. Kwenye Mipangilio ya iPhone, telezesha chini kisha uguse WhatsApp.
  2. Chini ya RUHUSU WHATSAPP IFIKIE, washa kipengele cha ufikiaji wa ruhusa. Unaweza pia kuchagua kuzuia ufikiaji wa ruhusa binafsi.
Ruhusa za picha na video
Ili kutumia picha na video zako kwenye WhatsApp, utahitaji kuipa programu ruhusa ya kufikia picha zako. Ukikataa kutoa ruhusa ya kutumia picha, utaona tahadhari hii:
  • "WhatsApp haina ruhusa ya kufikia picha au video zako. Ili uwashe ufikiaji, gusa Mipangilio kisha uwashe Picha."
Kutoa ruhusa
Unaweza kutoa ruhusa kwa kubadilisha mipangilio ya faragha ya iPhone yako.
  1. Nenda kwenye Mipangilio ya iPhone
    > Faragha.
  2. Gusa Picha > WhatsApp > Kusoma na Kuandika.
Fungua WhatsApp na sasa utaweza kutumia Picha zako za iPhone ulizonazo kwenye WhatsApp.
Ikiwa WhatsApp haipatikani au haionekani kwenye mipangilio ya faragha
Hakikisha kuwa huna vizuizi vyovyote ulivyoweka kwenye Mipangilio ya iPhone > Muda wa Kutumia Kifaa. Vinginevyo, unaweza kuhitaji kuhifadhi nakala na kurejesha simu yako.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La