Kuhusu ruhusa za WhatsApp

Android
iPhone
Unapotumia vipengele kwenye WhatsApp kwa mara ya kwanza, WhatsApp inaweza kuhitaji idhini ya kufikia maelezo au programu kwenye simu yako ya Android. Kuzima kipengele cha ruhusa kunaweza kusababisha WhatsApp ipoteze utendaji.
Ikiwa tayari umesakinisha WhatsApp, unaweza kudhibiti ruhusa ambazo programu inatumia kwenye mipangilio ya simu yako. Kulingana na simu yako ya Android, unaweza kufanya hii kwa njia kadhaa:
  • Fungua Mipangilio ya simu yako, kisha uguse Programu na arifa > WhatsApp > Ruhusa.
  • Fungua Mipangilio ya simu yako, kisha uguse Programu > Dhibiti programu > WhatsApp > Ruhusa za programu au Ruhusa Nyingine.
Ili kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyokusanya na kutumia data, kagua Sera yetu ya Faragha.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La