Kwa nini ninaona onyo la uwezekano wa kugunduliwa kwa hatari?

Wavuti na Kompyuta ya dawati
Code Verify huongeza safu ya ziada ya usalama kwenye ufumbaji wa mwisho hadi mwisho wakati watu wanatumia WhatsApp kwenye wavuti. Ikiwa umepakua kiendelezi cha kivinjari cha Code Verify, unaweza kuona onyo linalosema “Imeshindwa kuthibitisha ukurasa kwa sababu kuna kiendelezi kingine cha kivinjari. Zingatia kusitisha kiendelezi/viendelezi vingine kisha ujaribu tena.” Hali hii inaweza kutokea kwa sababu zifuatazo:
  • Una kiendelezi kingine kilichosakinishwa ambacho kinatatiza uwezo wetu wa kuthibitisha ukurasa.
  • Viendelezi vyako vingine vinavyotumika kwenye kivinjari huenda vinaweza kusoma au kurekebisha maudhui unayoyaona kwenye WhatsApp Web. Njia bora ya kuhakikisha usalama wa ujumbe wako kwenye WhatsApp Web ni kuzima viendelezi vyovyote vinavyosababisha onyo hili.
Ili kutatua tatizo hilo:
  • Jaribu kusitisha viendelezi vyako vingine, kufanya mchakato wa uthibitishaji tena na kuendelea kutumia viendelezi vyako vingine baada ya kumaliza. Huenda itakubidi upakie upya WhatsApp Web ili kuondoa onyo hili.
  • Hitilafu ikiendelea, zima viendelezi vyovyote ambavyo huna uhakika navyo unapotumia ukurasa. Huenda itakubidi upakie upya WhatsApp Web ili kuondoa onyo hili.
  • Ikiwa unaamini viendelezi vingine unavyovitumia, hakuna hatua inayohitajika.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La