Jinsi ya kupakua WhatsApp Desktop

Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
WhatsApp inaweza kutumika kwenye kompyuta bila kivinjari. Kusakinisha WhatsApp Desktop kwenye kompyuta yako, ipakue kutoka kwenye Duka la Microsoft, Duka la Programu la Apple au tovuti ya WhatsApp. WhatsApp Desktop itafanya kazi tu kwenye kompyuta zinazokidhi mahitaji ifuatayo ya mifumo ya uendeshaji:
  • Windows 8.1 au mpya zaidi
  • macOS 10.11 au mpya zaidi
Kwa mifumo mingine yote ya uendeshaji, unaweza kutumia WhatsApp Web kwenye kivinjari chako.
Kupakua WhatsApp Desktop
  1. Kwenye kivinjari cha kompyuta yako, nenda katika ukurasa wa Kupakua WhatsApp, kisha pakua .exe au faili ya .dmg.
  2. Mara upakuaji ukikamilika, fungua faili ya .exe au .dmg kisha ufuate maelekezo ili kukamilisha usakinishaji.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La