Jinsi ya kupakua WhatsApp Desktop

Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Mac
WhatsApp inaweza kutumika kwenye kompyuta bila kivinjari. Ili kusakinisha WhatsApp Desktop kwenye kompyuta yako, ipakue kwenye Duka la Microsoft au tovuti ya WhatsApp. WhatsApp Desktop itafanya kazi tu kwenye kompyuta zinazokidhi mahitaji yafuatayo ya mfumo wa uendeshaji:
  • Toleo la Windows 10.1 au matoleo mapya zaidi
  • Toleo la macOS 11 au matoleo mapya zaidi
Kwa mifumo mingine yote ya uendeshaji, unaweza kutumia WhatsApp Web kwenye kivinjari chako.
Kupakua WhatsApp Desktop
  1. Kwenye kivinjari cha kompyuta yako, nenda katika Ukurasa wa Kupakua WhatsApp.
  2. Pakua programu hiyo na ufuate vidokezo ili ukamilishe usakinishaji.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La