Jinsi ya kusimamia wasimamizi wa kikundi

Msimamizi yeyote katika kikundi anaweza kumfanya mshiriki awe msimamizi. Kikundi kinaweza kuwa na idadi isiyo na kikomo ya wasimamizi. Mtu aliyeanzisha kikundi hawezi kuondolewa na atabaki kuwa msimamizi isipokuwa akiondoka kwenye kikundi.
Kumfanya mshiriki kuwa msimamizi
  1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bonyeza Chaguo > Maelezo ya kikundi.
    • Au, chagua kikundi katika orodha yako ya Soga. Kisha, bonyeza Chaguo > Maelezo ya kikundi.
  2. Chagua mshiriki unayetaka kumfanya msimamizi.
  3. Bonyeza Chaguo > Fanya msimamizi wa kikundi.
Kuondoa msimamizi
  1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha bonyeza Chaguo > Maelezo ya kikundi.
    • Au, chagua kikundi katika orodha yako ya Soga. Kisha, bonyeza Chaguo > Maelezo ya kikundi.
  2. Chagua msimamizi unayetaka kumwondoa.
  3. Bonyeza Chaguo > Mwondoe kuwa msimamizi.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La