Jinsi ya kutii sera za Biashara na za Uuzaji katika WhatsApp

Kagua maktaba yetu ya maudhui ya msaada wa Jukwaa la WhatsApp Business hapa.
Tunataka biashara zifurahie manufaa yote ya kuwatumia wateja wao ujumbe kwa kutumia WhatsApp Business, inayojumuisha Jukwaa la WhatsApp Business na programu ya WhatsApp Business. Ili kuhakikisha mazungumzo salama na yenye ubora wa juu, ni muhimu kwa biashara na Watoa Huduma za Biashara wote waelewe sera za Biashara na Uuzaji kwenye WhatsApp.
Sera hizi mbili zinatumika kwenye WhatsApp Business. Kwa upana Sera ya Biashara husimamia matumizi yanayokubalika ya bidhaa za WhatsApp Business na kuweka matarajio ya kuhakikisha hali bora ya utumiaji kwa wateja. Inatusaidia kubainisha ni aina na wigo gani wa biashara inaruhusiwa kwenye jukwaa letu. Sera ya Uuzaji inatumika kuongoza ikiwa biashara zinaweza kuuza bidhaa na huduma zao ndani ya katalogi, ujumbe, jalada la biashara na violezo vya ujumbe.
Tunapendekeza kuwa kila mtu anayetumia WhatsApp Business asome sera zote za Biashara na Uuzaji kwenye WhatsApp, lakini pia tunaelewa kuwa wakati mwingine kuna maswali ya ziada kuhusu vipengele fulani vya sera, jinsi tunavyotekeleza sera au jinsi sera zinavyoathiri aina fulani za biashara.
Kutii Sera za Biashara na za Uuzaji
Biashara zinazouza bidhaa na huduma zilizopigwa marufuku na sera ya Uuzaji bado zinaweza kutumia WhatsApp Business kutuma ujumbe mradi zinatuma tu kwa mtagusano fulani wa kabla na baada ya mauzo.
Baadhi ya mifano ya shughuli za mauzo zisizokubalika ni:
 • Kutangaza bidhaa au huduma zilizopigwa marufuku kwenye jalada la biashara
 • Kuunda na kutuma violezo kwenye Jukwaa la WhatsApp Business kuhusu kuuza bidhaa au huduma ambazo haziruhusiwi
 • Kujihusisha na ununuzi au muamala wa bidhaa au huduma zilizopigwa marufuku kwenye mtandao wa WhatsApp, kama vile kukamilisha oda, kukusanya malipo ili kuanzisha ununuzi, kusasisha oda au kushiriki risiti
Tumetoa mifano kadhaa ya mtagusano unaokubalika na usiokubalika kati ya wateja na biashara zinazouza bidhaa au huduma zilizopigwa marufuku na Sera ya Uuzaji.
Mtagusano unaokubalika
 • Ufahamu: Kushiriki maelezo zaidi kuhusu bidhaa au huduma au kujibu maswali ya wateja
 • Ufahamu/Kuzingatia/Utunzaji: Kushiriki kuponi au tangazo na mtumiaji kwenye mawasiliano
 • Kuzingatia: Kushiriki kiungo cha tovuti au namba ya simu na mtumiaji ambaye angependa kununua bidhaa au huduma
Mtagusano usiokubalika
 • Ununuzi: Mtumiaji kuchagua bidhaa au huduma anazotaka kununua ndani ya mazungumzo na biashara kuchukua maelezo ya malipo kwenye WhatsApp
 • Ununuzi: Kutuma arifa ya risiti kufuatia uuzaji wa bidhaa au huduma iliyopigwa marufuku
Vikomo hivi vya kufanya miamala katika uuzaji wa bidhaa na huduma kwenye WhatsApp vinatumika tu kwa aina zilizopigwa marufuku katika Sera ya Uuzaji. Bidhaa au huduma yoyote ambayo inaruhusiwa kuuzwa kulingana na Sera ya Uuzaji, inaruhusiwa kwenye WhatsApp Business. Kwa mfano, fulana si bidhaa iliyowekewa vikwazo, kwa hivyo zinaweza kununuliwa kwa kutumia Jukwaa la WhatsApp Business au programu ya WhatsApp Business.
Kuanzisha mawasiliano na wateja
Kulingana na Sera yetu ya Biashara, biashara zinaweza tu kuwasiliana na mtu kwenye WhatsApp ikiwa mtu huyo:
 • ameipatia biashara namba yake ya simu ya mkononi
 • amekubali mawasiliano kati yake na biashara kupitia WhatsApp
Kuchanganya, kudanganya, kulaghai, kupotosha, kutuma taka, au kushtukiza watu kwa mawasiliano ya biashara ni ukiukaji wa Sera yetu ya Biashara. Zaidi ya hayo, biashara haziwezi kushiriki au kuwauliza watu washiriki namba kamili za kadi za malipo, namba za akaunti ya fedha, namba za kitambulisho cha binafsi au vitambulisho vingine nyeti.
Wateja lazima waamue kujiunga na soga na biashara ili biashara itume ujumbe wowote ulioanzishwa na biashara nje ya saa 24 kwenye Jukwaa la WhatsApp Business.
Kumbuka: Ikiwa mtumiaji atawasiliana na biashara ili kuuliza swali au kupata maelezo zaidi, hii haimaanishi kuwa ameamua kujiunga. Bado ni lazima biashara ipate uamuzi wa mtumiaji kujiunga ili aweze kupokea ujumbe kwenye WhatsApp siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu mahitaji ya uamuzi wa kujiunga na mbinu bora kwenye Sera ya Biashara.
Kupitia vikundi mahususi vya Sera ya Uuzaji
Baadhi ya vikundi vya sera ya Uuzaji ni changamano kuliko vingine. Huu hapa ni muhtasari wa jinsi ya kuepuka ukiukaji wa sera ya Uuzaji kwa baadhi ya vikundi hivyo.
Dawa, ziwe za kuandikiwa na daktari, za burudani, au nyinginezo
Haturuhusu biashara ambazo lengo kuu ni kuuza na kufanya miamala moja kwa moja katika uuzaji wa dawa. Kizuizi hiki kinahusu dawa zilizoagizwa na daktari na zile za kujinunulia, bila kujali hali za idhini kitaifa au kimataifa. Maduka ya dawa hayaruhusiwi kutangaza au kuuza dawa, vifaa vya matibabu na bidhaa nyingine zilizopigwa marufuku na Sera ya Uuzaji. Biashara hizi pia zimepigwa marufuku kutumia WhatsApp Business kutuma ujumbe wa huduma kwa wateja ambao hauhusiani na utoaji wa huduma za matibabu. Kwa mfano, mawasiliano kuhusu dawa za kuandikwa yanaweza kutumwa kati ya madaktari au wengine wanaotoa huduma za matibabu. Hata hivyo, mapendekezo yanayohusiana na dawa hayawezi kuuzwa moja kwa moja ndani ya jukwaa la WhatsApp.
Hata hivyo, maduka ya dawa yaliyo na maabara tofauti ya kimatibabu au huduma za utunzaji wa wagonjwa yanaweza kusajili huduma hizo kwenye WhatsApp Business mradi tu yawe yanakidhi mahitaji yafuatayo:
 • Jina la akaunti ya WhatsApp Business lirejelee huduma ya matibabu (kwa mfano, "Kliniki", "Maabara", "upimaji", au "chanjo".)
 • Tovuti ya biashara ieleze wazi kwamba inatoa chanjo na/au inatoa upimaji wa kimatibabu
Maduka ya dawa ambayo hutoa huduma za matibabu yataruhusiwa kutagusana na wateja kwa njia sawa na huduma nyingine za matibabu, kama vile huduma za daktari na hospitali. Watengenezaji na watoa huduma za afya ambao hawashiriki katika uuzaji wa moja kwa moja pia wanaruhusiwa.
Mifano ya shughuli za huduma za matibabu zilizoidhinishwa ni:
 • Kutuma arifa binafsi kuhusu kustahiki kwa mtu kupokea chanjo
 • Kupanga miadi ya majaribio na kuchanjwa
 • Kujibu maswali kuhusu majaribio na chanjo
 • Kuanzisha roboti ya mawasiliano ili kujibu maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu huduma za matibabu, ikiwa ni pamoja na maelezo na chanjo ya COVID-19
 • Kutuma utafiti wa baada ya ziara na ufuatiliaji wa miadi
Bidhaa zinazoweza kumezwa, zisizo salama
Virutubisho vimepigwa marufuku na Sera ya Uuzaji na haviruhusiwi kuuzwa ndani ya katalogi, Maduka, mazungumzo ya ujumbe, jalada la biashara na/au violezo vya ujumbe.
Baadhi ya mifano ya virutubisho visivyoruhusiwa ni:
 • Stiroidi za kujenga mwili
 • Chitosan
 • Comfrey
 • Dehydroepiandrosterone
 • Ephedra
 • Homoni za ukuaji wa binadamu
 • Vitafunwa na poda zenye protini
 • Vitamini
Huduma za dijitali
Huduma kama vile kuchaji simu za mkononi, vifurushi vya televisheni kupitia visimbuzi na vifurushi vya intaneti vinaruhusiwa kuuzwa kwenye WhatsApp.
Huduma za dijitali ambazo biashara yake kuu ni kutoa usajili, maudhui yanayoweza kupakuliwa au ufikiaji wa maktaba ya maudhui ya dijitali haziwezi kutumia WhatsApp. Kwa kuzingatia kila hali kivyake, tunaweza kuruhusu baadhi ya biashara kutumia Jukwaa la WhatsApp Business kwa uwezo mdogo kwa mawasiliano ya kibiashara.
Baadhi ya mifano ya huduma dijitali zisizokubalika ni:
 • Huduma za Usajili na Kitiririsha maudhui
 • Hifadhi kwenye wingu
 • Huduma za VPN
 • Sarafu ya michezo
 • Misimbo ya kupakua
 • Vitabu pepe
 • Vitabu vya kusikiliza
Sarafu halisi, ya kielektroniki au bandia
Pesa halisi hurejelea fedha taslimu au thamani inayolingana na pesa taslimu ambayo ina thamani halisi ya kifedha.
Baadhi ya mifano ya sarafu halisi zisizokubalika ni:
 • Dola za Kimarekani
 • Hundi
 • Kadi zinazolipiwa awali
 • Kadi za zawadi
Sarafu pepe hutolewa na mashirika ya binafsi na kwa kawaida hazina thamani halisi ya kifedha nje ya jumuiya mahususi.
Baadhi ya mifano ya sarafu za pepe ni:
 • Sarafu ya michezo
 • Sarafu dijitali
Sarafu bandia hurejelea fedha ghushi au hati ghushi za kifedha.
Pombe
Ikiwa wazo kuu la biashara ni uuzaji wa pombe (pamoja na vileo na vifaa vya kutengenezea pombe), haiwezi kutumia jukwaa la WhatsApp kuuza bidhaa hizi.
Hata hivyo, ikiwa biashara inauza pombe pamoja na bidhaa nyingine au vitu vinavyohusiana na vileo (kama vile glasi, majokofu, vishikilia chupa za mvinyo na vitabu au DVD kuhusu pombe) kama sehemu ya wazo lake la biashara, basi inaweza kutumia jukwaa la WhatsApp kutuma ujumbe usiohusiana na mauzo. Biashara hiyo haiwezi kuorodhesha pombe katika katalogi yake.
Silaha
Ikiwa wazo utendaji wa msingi wa biashara ni kutoa, kuuza au utumiaji wa silaha, risasi au vilipuzi, haiwezi kutumia jukwaa la WhatsApp kuuza bidhaa hizi.
Baadhi ya mifano ya silaha zilizopigwa marufuku ni:
 • Bunduki na vipuri vya bunduki
 • Bunduki za rangi
 • Bunduki za marisawa
 • Fataki
 • Kipuliza pilipili
 • Teza
 • Bustani za kufyatua bunduki
 • Maonyesho ya bunduki
Hata hivyo, ikiwa uuzaji wa silaha ni sehemu moja ya muundo wa biashara, au ikiwa biashara inatangaza mafunzo ya usalama au leseni za silaha halali, inaweza kutumia jukwaa la WhatsApp kutuma ujumbe ambao hauhusiani na mauzo. Biashara hiyo haiwezi kuorodhesha silaha, risasi na vilipuzi katika katalogi za bidhaa.
Ni juu ya biashara kutii sheria inayotumika. Kagua Sera ya Uuzaji ili upate orodha iliyosasishwa ya bidhaa na huduma ambazo zimepigwa marufuku kuuzwa au kutangazwa kwenye WhatsApp Business.
Mteja akianzisha mazungumzo kuhusu kununua bidhaa au huduma kutoka katika wigo ambao hauruhusiwi na sera ya Uuzaji, tafadhali mwambie mteja awasiliane nawe kupitia mfumo tofauti kwa mazungumzo ya aina hizo za bidhaa au huduma zilizo katika wigo uliopigwa marufuku.
Rasilimali zinazohusiana
Kuhusu Utekelezaji wa Sera ya Mfumo wa WhatsApp Business
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La