Jinsi ya kuunda na kudumisha katalogi

Katalogi iliyosasishwa huwarahisishia wateja kutagusana na biashara yako. Pia husaidia kuonyesha bidhaa na huduma zako mpya.
Kuongeza bidhaa au huduma kwenye katalogi yako
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business > Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi.
  • Ikiwa unaunda katalogi mpya, gusa Ongeza bidhaa mpya.
 2. Gusa aikoni ya buluu ya jumlisha au Ongeza bidhaa mpya. Kisha, gusa Ongeza Picha.
 3. Gusa Chagua Picha kupakia picha kutoka kwa Picha au Piga Picha kupiga picha mpya. Unaweza kupakia hadi picha 10.
 4. Toa jina la bidhaa au huduma. Pia unaweza kuweka taarifa za hiari kama vile bei, maelezo, kiungo cha tovuti na msimbo wa bidhaa au huduma kwa ajili ya bidhaa unayopakia.
 5. Gusa Hifadhi.
Kumbuka: Kuweka bei kwenye katalogi kunapatikana katika baadhi ya nchi pekee.
Kudhibiti bidhaa au huduma ambazo wateja wanaweza kuona
Kumbuka: Huenda bado usiweze kutumia kipengele hiki.
Kuficha bidhaa za katalogi
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business > Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi.
 2. Gusa bidhaa au huduma unazotaka kuficha > Zaidi
  > Hariri.
 3. Washa Ficha bidhaa hii.
 4. Gusa Hifadhi.
Au, telezesha kushoto kwenye bidhaa iliyo katika kidhibiti cha Katalogi. Kisha, gusa Ficha > Ficha.
Bidhaa ulizoficha bado zitaonekana kwenye kidhibiti chako cha katalogi zikiwa na
juu ya picha ya bidhaa. Ukifungua ukurasa wa maelezo ya bidhaa, pia utaona dondoo inayoonyesha kuwa umeficha bidhaa hii.
Kufichua bidhaa za katalogi
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business > Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi.
 2. Gusa bidhaa au huduma unayotaka kuifichua > Zaidi
  > Hariri.
 3. Zima Ficha bidhaa hii.
 4. Gusa Hifadhi.
Au, telezesha kushoto kwenye bidhaa iliyo katika kidhibiti cha Katalogi. Kisha, gusa Fichua > Fichua.
Futa bidhaa au huduma kutoka kwenye katalogi yako
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business > Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi.
 2. Telezesha kushoto kwenye bidhaa au huduma unayopenda kufuta. Kisha, gusa Futa > Futa.
Au, chagua picha ya bidhaa au huduma unayotaka kuifuta. Kisha, gusa Hariri > Futa > Futa.
Kumbuka:
 • Kila picha inayopakiwa kwenye katalogi itakaguliwa. Ukaguzi husaidia kuthibitisha kuwa picha, bidhaa au huduma zinakidhi Sera ya WhatsApp ya Uuzaji.
 • Ikiwa akaunti yako ya WhatsApp Business imeunganishwa na duka la Facebook na umeruhusu WhatsApp kuwa kituo cha mauzo, nafasi ya katalogi yako ya WhatsApp itachukuliwa na duka lako la Facebook kwa chaguomsingi. Hatua hii haitafuta au kubadilisha katalogi yako ya WhatsApp, lakini wewe na wateja wako hamtaiona. Unaweza kurudi kwenye katalogi yako ya WhatsApp wakati wowote kwa kuzima au kuficha WhatsApp isiwe kituo cha mauzo. Pata maelezo ya jinsi ya kudhibiti kituo chako cha mauzo kwenye Kidhibiti cha Biashara katika makala haya.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La