Jinsi ya kuangalia msimbo wako wa QR wa WhatsApp Business

Msimbo wako wa QR wa WhatsApp Business ni picha inayoweza kuchanganuliwa ambayo inawarahisishia wateja wako kukutumia ujumbe. Wateja wako wanahitaji tu kuchanganua msimbo wako na watapokea maelezo yako ya mawasiliano kiotomatiki.
Kuangalia msimbo wako wa QR wa WhatsApp Business
  1. Fungua programu ya WhatsApp Business > gusa Chaguo zaidi
    > Mipangilio.
  2. Gusa Msimbo wa QR karibu na jina lako, au gusa Zana za biashara > Kiungo kifupi > Angalia Msimbo wa QR.
Dokezo la Biashara: Ili iwe rahisi kwa wateja wako kukupata kwenye WhatsApp, chapisha nakala ya msimbo wako wa QR wa WhatsApp Business na uuweke wazi mahali panapoonekana.
Rasilimali zinazohusiana:
Kuhusu msimbo wa QR wa WhatsApp kwa ajili ya biashara
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La