Jinsi ya kuondoka kwenye kikundi na kufuta vikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Unaweza kuwafutia washiriki wote kikundi ikiwa wewe ni msimamizi wa kikundi husika. Kabla ya kufuta kikundi ni sharti uondoe washiriki wote wa kikundi, kisha uondoke kwenye kikundi.
Ukifuta kikundi, hutakiona tena katika orodha ya soga zako na historia ya soga itafutwa kwenye simu yako. Washiriki wengine bado wataona kikundi kwenye orodha ya soga zao. Hata hivyo, hamna atakayeweza kutuma ujumbe.
Kuondoa washiriki wa kikundi
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi. Au, gusa na ushikilie kikundi kwenye kichupo cha SOGA.
  2. Gusa jina la mshiriki > Mwondoe {participant} > Sawa.
Kuondoka kwenye kikundi
Baada ya kuondoa washiriki wote kwenye kikundi, unahitaji kuondoka kwenye kikundi.
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi. Au, gusa na ushikilie kikundi kwenye kichupo cha SOGA.
  2. Gusa Ondoka kwenye kikundi > ONDOKA.
Kufuta kikundi
Baada ya kuondoka kwenye kikundi, utakuwa na chaguo la kufuta kikundi hicho.
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
    • Au, gusa na ushikilie kikundi kwenye kichupo cha SOGA.
  2. Gusa Futa kikundi > FUTA.
    • Kama hutaki kufuta maudhui ya kikundi kutoka kwenye simu yako, hakikisha kuwa umeondoa uteuzi kwenye kisanduku cha Futa maudhui kwenye soga hii au Futa maudhui kwenye soga hizi.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La