Â
Jinsi ya kuweka au kuondoa soga au kikundi nyarakani
Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Mac
Kipengele cha kunyarakisha soga hukuruhusu kuficha soga ya binafsi au ya kikundi kutoka kwenye orodha ya soga zako ili kupanga vizuri mazungumzo yako.
Kumbuka:
- Kunyarakisha soga hakutafuta au kuhifadhi nakala ya soga husika kwenye kadi yako ya SD.
- Soga za binafsi au za kikundi zilizonyarakishwa zitabakia nyarakani utakapopokea ujumbe mpya kutoka kwa mtu huyo au soga ya kikundi.
- Hutapokea arifa za soga ambazo umezinyarakisha isipokuwa ikiwa umetajwa au kujibiwa.
Kunyarakisha soga ya binafsi au ya kikundi
- Kwenye kichupo cha Soga, gusa na ushikilie soga ambayo ungependa kuificha.
- Gusailiyo sehemu ya juu ya skrini.
Kunyarakisha soga zote
- Kwenye kichupo cha Soga, gusa > Mipangilio.
- Gusa Soga > Historia ya soga > Nyarakisha soga zote > Sawa.
Kuangalia soga za binafsi au za kikundi ambazo umezinyarakisha
- Sogeza hadi sehemu ya juu ya skrini ya Soga.
- GusaZilizonyarakishwa.
Namba iliyo karibu na
Zilizonyarakishwa huonyesha idadi ya soga za binafsi au za kikundi ambazo umezinyarakisha zilizo na ujumbe ambao hujasoma.

Kuondoa soga ya binafsi au ya kikundi nyarakani
- Sogeza hadi sehemu ya juu ya skrini ya Soga.
- GusaZilizonyarakishwa.
- Gusa na ushikilie soga ya binafsi au ya kikundi ambayo ungependa kuiondoa nyarakani.
- Gusa aikoni ya ondoa nyarakani iliyo sehemu ya juu ya skrini.
Mipangilio mbadala ya kunyarakisha
Kubadilisha mipangilio chaguomsingi ili soga zilizonyarakishwa ziondoke nyarakani ujumbe mpya unapopokelewa na uondoe
Zilizonyarakishwa ili zisionekane sehemu ya juu ya orodha ya soga zako:

- Kwenye kichupo cha Soga, gusa > Mipangilio.
- Gusa Soga.
- Zima Nyarakisha soga.