Kuhusu taka na ujumbe usiohitajika

Tunajizatiti ili kupunguza ujumbe wowote taka unaoweza kupitia kwenye mfumo wetu. Kuunda nafasi salama kwa watumiaji kuwasiliana na wenzao ni kipaumbele chetu na tunakusudia kupunguza ujumbe usiohitajika ambao unaweza kutumwa kwenye WhatsApp. Hata hivyo, sawa na SMS na kupiga simu kwa kawaida, inawezekana kwa watumiaji wengine wa WhatsApp walio na nambari yako ya simu kuwasiliana nawe na tunataka kukusaidia kutambua na kushughulikia aina hizi za ujumbe.
Ujumbe usiouhitaji unaweza kutoka au kutotoka kwa mmoja wa unaowasiliana nao. Aina hizi za ujumbe zinaweza kueneza taarifa potofu na kukufanya uamini taarifa isiyo sahihi.
Kutambua ujumbe usiohitajika
Kuna ishara zinazoweza kuonyesha umepokea ujumbe unaoshukiwa au kwamba mtumaji anajifanya kuwa mtu fulani ambaye siye. Angalia ujumbe ulio na yafuatayo, kwani yanaweza kuonyesha kuwa mtumaji si wa kuaminika:
  • Makosa ya tahajia au sarufi
  • Kukuomba uguse kiungo au uwashe kipengele kipya kupitia kiungo
  • Kukuomba utume taarifa zako za binafsi, kama vile nambari ya kadi ya mkopo au nambari ya akaunti ya benki, tarehe ya kuzaliwa, manenosiri
  • Kukuomba usambaze ujumbe
  • Kudai kuwa inabidi ulipie ili kutumia WhatsApp
Kumbuka, WhatsApp ni programu ya bure na huhitaji kulipia ili kuitumia.
Lakufanya kuhusu ujumbe usiohitajika
Ikiwa ujumbe unaonekana kuwa wa kutiliwa shaka au unaonekana kuwa mzuri sana kuliko ukweli, usiuguse, usiushiriki wala kuusambaza. Unapopokea aina hii ya ujumbe, tunapendekeza uripoti ujumbe huo, zuia mtumaji na ufute ujumbe huo. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuzuia na kuripoti waasiliani hapa. Unaweza pia kumwambia mwasiliani kuwa ujumbe unaonekana kuwa wa kutiliwa shaka na umfafanulie jinsi ya kutumia WhatsApp kwa uwajibikaji.
Ni mazoea bora, ikiwa huna uhakika kama kitu ni cha kweli au kama hujui ni nani aliyeandika ujumbe ulioupokea, tunapendekeza usiusambaze. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu kuzuia usambazaji wa taarifa potofu kwenye makala haya.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La