Udhibiti Unapowasiliana na Biashara

Udhibiti ni wako unapowasiliana na biashara kwenye WhatsApp. Ni wewe unaamua kama unataka au hutaki kushiriki nambari yako na biashara, pia unaweza kuzuia biashara wakati wowote. WhatsApp haiwezi kuipa biashara nambari yako, pia sera zetu zinakataza biashara kuwasiliana na wewe kwenye WhatsApp kabla ya kupokea idhini yako kufanya hivyo.
Kuzuia au kuripoti biashara
Unapopokea ujumbe kutoka kwenye biashara kwa mara ya kwanza, tutakupa chaguo la kuzuia au kuripoti biashara hiyo ikiwa hutaki kusikia kutoka kwao tena. Pia, wakati wowote wa mazungumzo na biashara, unaweza kuzuia au kuiripoti kutokea kwenye jalada lake.
Ukizuia akaunti ya biashara, unaweza pia kutuambia ni kwa nini, kwa mfano huhitaji tena kutuma ujumbe kwa biashara hiyo au hukujisajili kupokea ujumbe kutoka kwenye biashara hiyo. Pia tunaweza kutumia taarifa hizi za kuzuia na kuripoti ili kuchukua hatua dhidi ya akaunti au kupunguza idadi ya ujumbe inayoweza kutumwa na biashara husika.
Kushiriki maoni kuhusu ujumbe
Pia una chaguo la kutoa maoni kuhusu ujumbe wa binafsi ambao biashara zinakutumia.
  1. Fungua WhatsApp.
  2. Kisha, fungua soga kati yako na biashara hiyo.
  3. Gusa na ushikilie ujumbe unaotaka kuukadiria.
  4. Gusa Kadiria.
  5. Chagua idadi ya nyota ili kutathmini ujumbe.
  6. Gusa Wasilisha.
Tunaweza pia kutumia mrejesho huu ili kusaidia biashara kuboresha soga zao na wateja. Mrejesho huu ni wa asiyejulikana, ikiwa inamaanisha kuwa biashara na WhatsApp haziwezi kuona ni nani aliyeyatoa. WhatsApp haioni maudhui ya ujumbe wako na biashara.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La