Imeshindwa kuhamisha historia ya soga kutoka kwenye Android hadi kwenye iPhone

Kuhamisha historia yako ya soga za WhatsApp kutoka kwenye simu ya Android kwenda kwenye iPhone, lazima uwe na yafuatayo:
 • Android OS Lollipop, SDK 21 au mpya zaidi au Android 5 au toleo jipya zaidi liwe limesakinishwa kwenye kifaa chako cha Android
 • iOS 15.5 au mpya zaidi iwe imesakinishwa kwenye iPhone yako
 • Programu ya Move to iOS iliyosakinishwa kwenye simu yako ya Android
 • Toleo la WhatsApp 2.22.10.70 au jipya zaidi kwenye kifaa chako kipya
 • Toleo la WhatsApp Android 2.22.7.74 au jipya zaidi kwenye kifaa chako cha zamani
 • Tumia namba ile ile ya simu kwenye simu yako ya zamani na katika kifaa chako kipya
 • iPhone yako lazima iwe mpya kama ilivyotoka kiwandani au weka upya mipangilio ya kiwandani ili kuoanisha na programu ya Move to iOS na kuhamisha data kutoka kwa simu yako ya Android
 • Vifaa vyako vyote viwili lazima viwe vimeunganishwa kwenye chanzo cha nishati
 • Vifaa vyako vyote viwili vinahitaji kuunganishwa kwenye mtandao sawa wa Wi-Fi au utahitaji kuunganisha kifaa chako cha Android kwenye mtandao pepe wa iPhone yako
WhatsApp tayari inafanya kazi, imeruka au imekosa chaguo muhimu kwenye kifaa changu kipya
Unaweza tu kurejesha historia yako ya WhatsApp kabla ya kuanza kutumia WhatsApp kwenye kifaa chako kipya. Ikiwa unataka kurudisha historia ya ujumbe wako wa zamani, unaweza:
 1. Kufuta WhatsApp kutoka kwenye iPhone yako.
 2. Kusajili upya WhatsApp kwenye Android yako.
 3. Kuanzisha uhamishaji mpya ukitumia Move to iOS kwenye simu yako ya Android.
Kumbuka: Haiwezekani kuunganisha historia mpya na ya zamani.
Kifaa changu kipya kina namba tofauti ya simu
Haiwezekani kuhamisha data yako ya WhatsApp kwenda kwenye namba mpya ya simu. Hata hivyo, unaweza kubadilisha namba yako ya simu kwenye kifaa chako cha zamani kuwa namba yako mpya kabla ya kuhamia kwenye simu yako mpya.
Pata maelezo ya jinsi ya kubadilisha namba yako ya WhatsApp kwenye kifaa chako cha zamani katika makala haya.
Programu ya Move to iOS imeacha kufanya kazi au umeshindwa
Ukikumbana na matatizo na programu ya Move to iOS, tafadhali wasiliana na Usaidizi wa Apple.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La