Kuhusu anwani na programu yako ya WhatsApp Business

GDPR na nambari zilizo kwenye kitabu chako cha anwani
Unapotumia programu ya WhatsApp Business, wewe ndiwe Mdhibiti wa anwani zote zilizo kwenye kitabu cha anwani cha kifaa chako. Kama Mdhibiti, lazima uwe na msingi wa kisheria wa kuchakata anwani ulizo nazo, iwe ni kwa lengo la kutimiza mkataba, kwa mujibu wa masilahi halali, idhini, au msingi mwingine wowote sahihi wa kisheria ulioelezwa katika Kifungu cha 6 cha GDPR.
Unapoipatia WhatsApp ufikiaji wa anwani hizo, WhatsApp inakuwa Mchakataji wako wa data. Tunaamua kwa haraka ikiwa unaweza kutuma ujumbe kwenye anwani hizo katika WhatsApp kisha tunawasilisha ujumbe wako kwa wapokeaji uliokusudia. Kwa maelezo zaidi, rejelea Masharti ya WhatsApp Business ya Uchakataji wa Data yaliyotajwa na kujumuishwa ndani ya Masharti yetu Huduma ya WhatsApp Business.
Dhibiti na usimamie ufikiaji wa kitabu chako cha anwani
Kuna njia kadhaa za kudhibiti ni anwani gani unazotoa kwa WhatsApp. Kwa mfano, unaweza kuongeza tu anwani ambazo una msingi sahihi wa kisheria kwenye kitabu cha anwani cha kifaa chako. Faida moja ya njia hii ni kwamba inakuhimiza wewe na wafanyakazi wako kudumisha desturi bora za faragha ya data. Kuweka mawasiliano ya biashara pamoja na vifaa tofauti na vile vya binafsi husaidia kuzuia matumizi mabaya ya data ya wateja au vifaa vya kampuni kwa matumizi ya binafsi (na kinyume chake).
Ikiwa unataka kuweka mawasiliano yako yote ya biashara na ya binafsi kwenye kifaa kimoja, unaweza kugawanya kitabu chako cha anwani kwa kutumia zana zinazoruhusu kuwa na vitabu tofauti vya anwani.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La