Jinsi ya kufuta ujumbe

Android
iOS
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Mac
Unaweza kufuta ujumbe kwako tu au uombe ujumbe huo ufutwe kwa kila mtu. Iwapo ungependa kuhariri ujumbe badala yake, unaweza kuhariri kwa hadi dakika 15 baada ya kutuma.
Unapofuta ujumbe, hakuna njia ya kuurejesha isipokuwa kama umejumuisha ujumbe huo kwenye nakala.
Kufuta ujumbe kwa kila mtu
Kufuta ujumbe kwa kila mtu hukuruhusu kufuta ujumbe mahususi ambao umetuma kwenye soga ya binafsi au ya kikundi. Kitendo hiki ni muhimu hasa ikiwa umetuma ujumbe kwenye soga isiyo sahihi au ikiwa ujumbe ambao umetuma una makosa. Kama msimamizi wa kikundi, unaweza kuondoa ujumbe wenye hitilafu ambao umetumwa na washiriki wengine kwenye soga.
Nafasi ya ujumbe uliotuma ambao umefuta kwa kila mtu itawakilishwa na:
"Umefuta ujumbe huu"
Kufuta ujumbe ambao umetuma kwa kila mtu
 1. Fungua WhatsApp kisha uende kwenye soga iliyo na ujumbe ambao ungependa kuufuta.
 2. Gusa na ushikilie ujumbe > chagua Futa kwenye menyu. Au chagua ujumbe zaidi ili uweze kufuta ujumbe nyingi kwa wakati mmoja.
  • Ukiulizwa, gusa
   more
   > chagua Futa kwenye menyu.
 3. Gusa
  delete message
  > Futa kwa Kila Mtu.
Wasimamizi wa kikundi wanaweza kufuta ujumbe ambao umetumwa na mshiriki mwingine wa kikundi. Hatua hii huwawezesha wasimamizi kudhibiti vikundi na jumuiya zao binafsi kwa kufuta ujumbe au maudhui yasiyofaa kwa washiriki wote. Msimamizi anapofuta ujumbe kwa kila mtu, nafasi ya ujumbe huwakilishwa na:
“Ujumbe huu umefutwa na msimamizi [jina la msimamizi]”
Kufuta ujumbe uliotumwa na mshiriki mwingine wa kikundi
 1. Fungua WhatsApp kisha uende kwenye soga iliyo na ujumbe ambao ungependa kuufuta.
 2. Gusa na ushikilie ujumbe husika.
 3. Gusa
  delete message
  > Futa kwa Kila Mtu > Futa.
Dokezo:
 • Ni lazima wewe pamoja na wapokeaji wa ujumbe muwe mnatumia toleo la hivi karibuni la WhatsApp.
 • Huenda wapokeaji wanaotumia toleo la WhatsApp la iOS bado wanaweza kuwa na maudhui uliyoyatuma yakiwa yamehifadhiwa kwenye Picha zao, hata baada ya kufuta ujumbe husika kwenye soga ya WhatsApp.
 • Wapokeaji wanaweza kuona ujumbe wako kabla haujafutwa au ikiwa ufutaji haukukamilika.
 • Hutaarifiwa ikiwa ufutaji haukukamilika kwa kila mtu.
 • Una siku mbili baada ya kuutuma ujumbe kuomba Kufuta kwa Kila Mtu.
 • Wasimamizi wa kikundi pekee ndio wanaweza kufuta ujumbe uliotumwa na washiriki wengine wa kikundi.
 • Wasimamizi wa kikundi wana siku mbili baada ya mtu kuutuma ujumbe kuomba Kufuta kwa Kila Mtu.
 • Washiriki wa kikundi wataweza kuona ni msimamizi gani aliyechagua Futa kwa Kila Mtu.
 • Ujumbe unaofutwa na msimamizi wa kikundi hauwezi kurejeshwa wala kukatiwa rufaa.
Kujifutia ujumbe
Unaweza kufuta nakala ya ujumbe wako ambao umetuma au kupokea kwenye simu yako. Hatua hii haina athari kwa soga za wapokeaji wako. Wapokeaji wako bado wataona ujumbe husika katika skrini zao za soga.
 1. Fungua WhatsApp kisha uende kwenye soga iliyo na ujumbe ambao ungependa kuufuta.
 2. Gusa na ushikilie ujumbe husika > kisha uguse
  delete message
  > Futa Kwangu. Au chagua ujumbe zaidi ili uweze kufuta ujumbe nyingi kwa wakati mmoja.
Kumbuka: Baada ya kuchagua Futa kwangu, una hadi sekunde 5 kutendua kitendo hiki kwa kubonyeza Tendua kabla ya ujumbe kufutwa kabisa.
Kufuta maudhui kwenye soga
Unaweza kufuta nakala ya maudhui yako ambayo umetuma au kupokea kwenye simu yako. Hatua hii haina athari kwa soga za wapokeaji wako. Wapokeaji wako bado wataona maudhui husika katika skrini zao za soga.
 1. Gusa na shikilia faili ya maudhui.
 2. Gusa
  delete message
  .
 3. Baada ya kuchagua ujumbe wa kwanza, unaweza kuchagua ujumbe mwingine wa kufuta kabla ya kugusa
  delete message
  .
Hakuna namna ya kufuta midia zote kutoka kwenye soga kwa hatua moja. Namna rahisi ya kufuta midia nyingi ni kufanya yafuatayo:
 1. Fungua soga.
 2. Gusa jina la soga ili kuingiza maelezo ya soga ya skrini.
 3. Gusa Maudhui, Viungo na Hati.
 4. Gusa Chagua.
 5. Gusa maudhui yoyote ili kuyaongeza kwenye uteuzi wako.
 6. Gusa
  delete message
  .
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La