Jinsi ya kufuta ujumbe

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Unaweza kufuta ujumbe kwako mwenyewe au kuomba ujumbe ufutwe kwa kila mtu.
Kufuta ujumbe kwa kila mtu
Kufuta ujumbe kwa kila mtu hukuruhusu ufute ujumbe mahususi uliotuma kwenye soga ya binafsi au ya kikundi. Hii ni muhimu hasa ikiwa ulituma ujumbe kwenye soga isiyo sahihi au kama ujumbe uliotuma una makosa. Ukiwa msimamizi wa kikundi, umewezeshwa pia kuondoa ujumbe usiofaa au wenye matatizo kwenye soga.
Nafasi ya ujumbe uliotuma ambao umefutwa kwa kila mtu itachukuliwa na:
Umefuta ujumbe huu
Kufuta ujumbe ulioutuma kwa kila mtu:
 1. Fungua WhatsApp kisha uende kwenye soga iliyo na ujumbe unaotaka kuufuta.
 2. Gusa na ushikilie ujumbe husika > chagua Futa kwenye menyu. Ukipenda, chagua ujumbe zaidi ili kufuta ujumbe kadhaa kwa wakati mmoja.
  • Ukiulizwa, gusa Zaidi
   > chagua Futa kwenye menyu.
 3. Gusa Futa
  > Futa kwa Kila Mtu.
Ikiwa wewe ni msimamizi wa kikundi, unaweza kufuta ujumbe uliotumwa na mshiriki mwingine wa kikundi. Hatua hii huwawezesha wasimamizi kudhibiti vikundi vyao binafsi na jumuiya kwa kufuta ujumbe wa matusi au wenye maudhui yasiyofaa kwa washiriki wote. Msimamizi anapofuta ujumbe kwa kila mtu, nafasi ya ujumbe itachukuliwa na:
“Ujumbe huu ulifutwa na msimamizi, [jina la msimamizi]”
Ili kufuta ujumbe uliotumwa na mshiriki mwingine wa kikundi:
 1. Fungua WhatsApp kisha uende kwenye soga iliyo na ujumbe unaotaka kuufuta.
 2. Gusa na ushikilie ujumbe husika.
 3. Gusa Futa
  > Futa kwa Kila Mtu > SAWA.
Kumbuka:
 • Ili ujumbe ufutwe kwa kila mtu, wewe na wapokeaji lazima muwe mnatumia toleo la karibuni la WhatsApp.
 • Wapokeaji wanaotumia toleo la WhatsApp la iOS bado wanaweza kuwa na maudhui uliyotuma yakiwa yamehifadhiwa kwenye Picha zao, hata baada ya kufutwa kwenye soga ya WhatsApp.
 • Wapokeaji wanaweza kuona ujumbe kabla haujafutwa au kama ufutaji haukukamilika.
 • Hutaarifiwa iwapo ufutaji haukufanikiwa kwa kila mtu.
 • Una kama siku 2 baada ya kutuma ujumbe kuomba Kufuta kwa Kila Mtu.
 • Wasimamizi wa kikundi pekee ndio wanaoweza kufuta ujumbe unaotumwa na washiriki wengine wa kikundi.
 • Wasimamizi wa kikundi wana siku 2 baada ya mtu kutuma ujumbe kuomba Kufuta kwa kila mtu.
 • Washiriki wa kikundi wataweza kuona ni msimamizi gani alichagua Kufuta kwa Kila Mtu.
 • Ujumbe uliofutwa na msimamizi wa kikundi hauwezi kurejeshwa na hauwezi kukatiwa rufaa.
Kujifutia ujumbe
Unaweza kufuta nakala ya ujumbe wako uliotuma au kupokea kwenye simu yako. Hatua hii haina athari kwa soga za wapokeaji wako. Wapokeaji wako bado wataona ujumbe katika skrini zao za soga.
Kujifutia ujumbe:
 1. Fungua WhatsApp kisha uende kwenye soga iliyo na ujumbe unaotaka kuufuta.
 2. Gusa na ushikilie ujumbe husika > chagua Futa kwenye menyu. Ukipenda, chagua ujumbe zaidi ili kufuta ujumbe kadhaa kwa wakati mmoja.
  • Ukiulizwa, gusa Zaidi
   > chagua Futa kwenye menyu.
 3. Gusa Futa
  iliyo juu ya skrini > Futa Kwangu.
Kumbuka: Baada ya kuchagua Futa kwangu, una sekunde 5 kutendua kitendo hiki kwa kubonyeza Tendua kabala ya ujumbe kufutwa kabisa.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kufuta ujumbe: Android | KaiOS
Jinsi ya kufuta soga: Android | iPhone
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La