Jinsi ya kufuta ujumbe
Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Unaweza kufuta ujumbe kwako mwenyewe au kuomba ujumbe ufutwe kwa kila mtu.
Kufuta ujumbe kwa kila mtu
Kufuta ujumbe kwa kila mtu hukuruhusu ufute ujumbe mahususi uliotuma kwenye soga ya binafsi au ya kikundi. Hii ni muhimu hasa ikiwa ulituma ujumbe kwenye soga isiyo sahihi au kama ujumbe uliotuma una makosa. Ukiwa msimamizi wa kikundi, umewezeshwa pia kuondoa ujumbe wenye hitilafu au matatizo unaotumwa na washiriki wengine kwenye soga.
Nafasi ya ujumbe uliotuma ambao umefutwa kwa kila mtu itachukuliwa na:
“Ujumbe huu umefutwa”
Kufuta ujumbe ulioutuma kwa kila mtu:
- Fungua WhatsApp kisha uende kwenye soga iliyo na ujumbe unaotaka kuufuta.
- Gusa na ushikilie ujumbe husika. Ukipenda, chagua ujumbe zaidi ili kufuta ujumbe kadhaa kwa wakati mmoja.
- Gusa Futa> Futa kwa Kila Mtu.
Ikiwa wewe ni msimamizi wa kikundi, unaweza kufuta ujumbe uliotumwa na mshiriki mwingine wa kikundi. Hatua hii huwawezesha wasimamizi kudhibiti vikundi vyao binafsi na jumuiya kwa kufuta ujumbe wa matusi au wenye maudhui yasiyofaa kwa washiriki wote. Msimamizi anapofuta ujumbe kwa kila mtu, nafasi ya ujumbe itachukuliwa na:
“Ujumbe huu ulifutwa na msimamizi, [jina la msimamizi]”
Ili kufuta ujumbe uliotumwa na mshiriki mwingine wa kikundi:
- Fungua WhatsApp kisha uende kwenye soga iliyo na ujumbe unaotaka kuufuta.
- Gusa na ushikilie ujumbe husika.
- Gusa Futa> Futa kwa kila mtu > SAWA.
Kumbuka:
- Ili ujumbe ufutwe kwa kila mtu, wewe na wapokeaji lazima muwe mnatumia toleo la karibuni la WhatsApp.
- Wapokeaji wanaotumia toleo la WhatsApp la iOS bado wanaweza kuwa na maudhui yaliyotumwa kwenye Picha zao, hata baada ya kufutwa kwenye soga za WhatsApp.
- Wapokeaji wanaweza kuona ujumbe kabla haujafutwa au kama ufutaji haukukamilika.
- Hutaarifiwa kama ufutaji haukufanikiwa kwa kila mtu.
- Una kama siku 2 baada ya kutuma ujumbe kuomba Kufuta kwa Kila Mtu.
- Wasimamizi wa kikundi pekee ndio wanaweza kufuta ujumbe uliotumwa na washiriki wengine wa kikundi.
- Wasimamizi wa kikundi wana kama siku 2 baada ya mtu mwingine kutuma ujumbe kuomba Kufuta kwa Kila Mtu.
- Washiriki wa kikundi wataweza kuona ni msimamizi yupi aliyechagua Kufuta kwa Kila Mtu.
- Ujumbe uliofutwa na msimamizi wa kikundi hauwezi kurejeshwa na hauwezi kukatiwa rufaa.
Kujifutia ujumbe
Unaweza kufuta nakala ya ujumbe wako uliotuma au kupokea kwenye simu yako. Hatua hii haina athari kwa soga za wapokeaji wako. Wapokeaji wako bado wataona ujumbe katika skrini zao za soga.
Kujifutia ujumbe:
- Fungua WhatsApp kisha uende kwenye soga iliyo na ujumbe unaotaka kuufuta.
- Gusa na ushikilie ujumbe husika. Ukipenda, gusa ujumbe zaidi ili kufuta ujumbe kadhaa kwa wakati mmoja.
- Gusa Futailiyo juu ya skrini > Futa kwangu.
Kumbuka: Baada ya kuchagua Futa kwangu, una sekunde 5 kutendua kitendo hiki kwa kubonyeza Tendua kabla ya ujumbe kufutwa kabisa.
Rasilimali zinazohusiana: