Jinsi ya kupakua programu ya WhatsApp Business

Android
iPhone
Programu ya WhatsApp Business ni programu inayoweza kupakuliwa bila malipo kwa ajili ya biashara ndogo.
Kabla ya kupakua programu, tafadhali fahamu yafuatayo:
  • Ikiwa una akaunti ya WhatsApp Messenger, unaweza kuhamisha taarifa za akaunti yako kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na historia ya soga na maudhui, kwenye akaunti mpya ya WhatsApp Business.
  • Historia yako ya soga haiwezi kurudishwa kwenye WhatsApp Messenger ukiamua kuacha kutumia programu ya WhatsApp Business.
  • Unaweza kutumia programu ya WhatsApp Business na pia WhatsApp Messenger wakati huo huo ilimradi akaunti ziwe zimeunganishwa na namba tofauti za simu. Haiwezekani kuwa na namba moja ya simu inayohusishwa na programu zote mbili kwa wakati mmoja.
Ili usakinishe programu ya WhatsApp Business:
  1. Pakua programu ya WhatsApp Business kutoka kwenye Duka la Programu la Apple.
  2. Thibitisha namba yako ya simu ya biashara.
  3. Ukipenda, rejesha yaliyo kwenye nakala uliyohifadhi.
  4. Weka jina lako la biashara.
  5. Unda jalada lako. Gusa Mipangilio > jina la biashara yako.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La