Jinsi ya kujisajili kwenye programu ya WhatsApp Business

Mahitaji
 • Unaweza tu kusajili simu ya mkononi au namba ya simu ya mezani (isiyosogea) unayomiliki.
 • Ni lazima uweze kupokea simu au SMS kwenye namba ya simu unayojaribu kusajili.
 • Hakikisha unatumia namba ya simu inayoruhusiwa. Namba za simu zisizoruhusiwa haziwezi kusajiliwa kwenye WhatsApp, namba hizo ni pamoja na:
 • VoIP
 • Namba zisizolipiwa
 • Namba za kulipia unapopigia
 • Namba za ufikiaji wa jumla (UAN)
 • Namba za binafsi
 • Ni lazima uwe umezima mipangilio ya kuzuia simu, programu au vizuia majukumu.
 • Ikiwa unajisajili kupitia simu yako ya mkononi, ni lazima uwe na muunganisho wa intaneti unaofanya kazi unatokana na data ya simu za mkononi au Wi-Fi. Ikiwa unatumia mtandao wa ng'ambo au una muunganisho mbaya, huenda usajili hautafanyika. Jaribu kufungua https://www.whatsapp.com/business/ kwenye kivinjari cha simu yako ya mkono ili uone kama umeunganishwa kwenye intaneti.
 • Ikiwa unajisajili kupitia simu ya mezani, gusa Nipigie kuomba upigiwe simu ili upokee msimbo wa usajili.
Jinsi ya kusajili
 1. Weka namba yako ya simu:
  • Chagua nchi yako kutoka kwenye orodha kunjuzi. Kufanya hivyo kutajaza kiotomatiki msimbo wa nchi upande wa kushoto.
  • Weka namba yako ya simu kwenye sanduku lililo upande wa kulia. Usiweke 0 kabla ya namba yako ya simu.
 2. Gusa Nimemaliza ili kupokea msimbo wa usajili. Ukiulizwa, unaweza pia kugusa Nipigie ili upokee msimbo kwa kupigiwa simu.
 3. Weka msimbo wa usajili wenye tarakimu 6 unaoupokea kupitia SMS au kwa kupigiwa simu.
  • Kumbuka: Ikiwa unatumia Ufunguo wa iCloud na uliwahi kusajili namba hii hapo awali, unaweza kusajiliwa kiotomatiki bila kupokea msimbo wa SMS.
Kutumia namba za viendelezi vya simu ya mezani
Namba za viendelezi vya simu ya mezani haziwezi kutumika kukamilisha mchakato wa usajili. Tafadhali tumia namba ya simu ya mezani isiyo na kiendelezi kuthibitisha namba yako ya simu. Kwa sababu za usalama, tunaweza tu kutuma msimbo wa usajili wenye tarakimu sita kwenye namba ya simu ya mezani unayotaka kutumia katika akaunti yako ya biashara.
Ikiwa hupokei msimbo wenye tarakimu sita kupitia SMS
 • Subiri upau wa maendeleo umalize kisha ujaribu tena. Muda wa kusubiri unaweza kuchukua hadi dakika 10.
 • Usikisie msimbo la sivyo utafungiwa kwa muda fulani.
 • Muda ukiisha kabla ya kupokea msimbo wa usajili, utaone chaguo la kuomba upigiwe simu. Chagua Nipigie ili uombe upigiwe simu. Unapopokea simu, sauti ya kiotomatiki itakuambia msimbo wa usajili wenye tarakimu 6. Weka msimbo huu kwenye programu ya WhatsApp Business.
  • Kumbuka: Kutegemeana na mtoa huduma wako, unaweza kutozwa gharama ya SMS na kupigiwa simu.
Hatua za utatuaji
Ikiwa una matatizo ya kusajili, jaribu yafuatayo:
 1. Zima simu yako, subiri sekunde 30 kisha uiwashe tena.
 2. Futa na usakinishe tena toleo la hivi karibuni la WhatsApp Business linalopatikana hapa.
 3. Angalia ikiwa unaweza kupokea ujumbe kwa kutuma SMS ya jaribio kutoka kwenye simu yoyote ya mkononi kwenda kwenye namba ya simu ya mkononi unayojaribu kusajili. Weka namba ya simu ya mkononi kama ulivyoiweka katika programu ya WhatsApp Business, ikijumuisha msimbo wa nchi.
  • Kumbuka: Hatuwezi kukutumia msimbo wako wa usajili kupitia njia nyingine kwa sababu za usalama.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La