Jinsi ya kutumia WhatsApp kwa uwajibikaji


WhatsApp imeundwa kuwa njia rahisi, salama na ya uhakika ya kutuma ujumbe kwa watu wengine. Kwa asili, kutuma ujumbe huwa kwa faragha na Masharti yetu ya Huduma yameundwa ili kukusaidia kuweka jukwaa letu na watumiaji wetu salama. Watumiaji wote wa WhatsApp wanapaswa kukagua miongozo ifuatayo ili kuhakikisha wanatumia WhatsApp kwa kuwajibika.
Mbinu bora
  • Wasiliana na watu unaowajua: Tuma tu ujumbe kwa wale ambao wamewasiliana nawe kwanza au wamekuomba uwasiliane nao kupitia WhatsApp. Ni bora kuwapa waasiliani nambari yako ya simu ili waweze kukutumia ujumbe kwanza.
  • Omba ruhusa na uheshimu mipaka: Pata ruhusa kwanza kutoka kwa waasiliani kabla ya kuwaongeza kwenye kikundi. Ukimwongeza mtu kwenye kikundi na akijiondoa, heshimu uamuzi wake.
  • Tumia vidhibiti vya kikundi: Tumeunda mipangilio ya wasimamizi pekee kwa ajili ya ujumbe kwa vikundi vya WhatsApp. Ikiwa wewe ni msimamizi, unaweza kuamua kama washiriki wote au wasimamizi wa kikundi pekee ndio wanaoweza kutuma ujumbe kwenye kikundi. Kutumia kipengele hiki kunaweza kusaidia kupunguza ujumbe usiohitajika katika vikundi. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kubadilisha mipangilio ya wasimamizi wa kundi kwenye Android, iPhone, KaiOS au Web na Desktop.
  • Tafakari kabla ya kusambaza ujumbe: Tumeunda lebo kwa ujumbe wote uliosambazwa na kiwango cha mara unachoweza kusambaza ujumbe kama njia ya kuhimiza watumiaji kutafakari kabla ya kushiriki. Ikiwa huna hakika kama kitu ni kweli au hujui ni nani aliyeandika ujumbe huo, tunapendekeza usisambaze. Pata maelezo zaidi kuhusu kuzuia kusambaa kwa taarifa potofu kwenye makala haya.
Mazoea ya kuepuka
Kutumia WhatsApp kwa njia yoyote iliyoorodheshwa hapa chini kunaweza kusababisha akaunti yako ipigwe marufuku.
  • Ujumbe usiohitajika: Mwasiliani akikuomba uache kumtumia ujumbe, unapaswa kumwondoa mtumiaji huyo kwenye kitabu chako cha anwani na uache kuwasiliana naye.
  • Ujumbe wa kiotomatiki au kutuma ujumbe kwa wingi: Usitume ujumbe kwa wingi, ujumbe wa kiotomatiki au kupiga simu kiotomatiki kwa kutumia WhatsApp. WhatsApp hutumia teknolojia ya mashine kujifunza na kuripoti kutoka kwa watumiaji ili kuchunguza na kupiga marufuku akaunti zinazotuma ujumbe usiohitajika. Pia, usifungue akaunti au kuunda vikundi kwa njia zisizoidhinishwa au za kiotomatiki au kutumia matoleo yaliyorekebishwa ya WhatsApp. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi WhatsApp inavyozuia matumizi mabaya ya ujumbe kutumwa kiotomatiki na kwa wingi, unaweza kusoma waraka huu rasmi.
  • Kutumia orodha za anwani ambazo si zako: Usishiriki namba za simu bila idhini au kutumia data zilizopatikana kutoka vyanzo visivyo halali kutuma ujumbe kwa watumiaji kwenye WhatsApp au kuwaongeza kwenye vikundi.
  • Kutumia orodha za matangazo kupita kiasi: Ujumbe uliotumwa kwa kutumia orodha ya tangazo utapokelewa tu wakati watumiaji wameweka nambari yako ya simu kwenye orodha yao ya waasiliani. Tafadhali kumbuka, matumizi ya mara kwa mara ya ujumbe wa matangazo yanaweza kusababisha watu kuripoti ujumbe wako na huwa tunapiga marufuku akaunti ambazo zinaripotiwa mara nyingi.
  • Kupakua taarifa binafsi: Epuka kupakua taarifa kutoka kwenye WhatsApp katika kiwango cha chini kabisa, kwa kutumia zana ya kiotomatiki au kwa kujifanyia, kwa madhumuni yoyote ambayo hayaruhusiwi. Kupata taarifa kutoka kwa watumiaji kwa njia hii, ikiwa ni pamoja na namba za simu, picha za jalada na hali kutoka kwenye WhatsApp kunakiuka Masharti yetu ya Huduma.
  • Kukiuka Masharti yetu ya Huduma: Kumbuka kwamba, Masharti yetu ya Huduma yanakataza, pamoja na mambo mengine, kuchapisha uongo na kuhusika katika vitendo vilivyo kinyume na sheria, vitisho, chuki na tabia za kukera za kikabila. Unaweza kuangalia Masharti yetu ya Huduma hapa.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La