Jinsi ya kuwa salama kwenye WhatsApp

Usalama na ulinzi wako na wa ujumbe wako ni muhimu kwetu. Tunataka ujue kuhusu zana na vipengele ambavyo tumeunda ili kukusaidia kuwa salama unapotumia WhatsApp.
Masharti Yetu ya Huduma
Njia moja tunayokusudia kuwa salama kwenye WhatsApp ni kupitia Masharti yetu ya Huduma. Masharti yetu ya Huduma yanabainisha shughuli zilizopigwa marufuku, ambazo ni pamoja na kushiriki maudhui (kwenye hali, picha ya jalada au ujumbe) ambayo ni kinyume cha sheria, ya aibu, ya kukashifu, ya kutisha, ya kunyanyasa, ya chuki, ya kukera na ya kikabila au yanayochochea au kuhimiza mwenendo ambao ni kinyume cha sheria au vinginevyo hayafai au yanakiuka Masharti yetu ya Huduma. Tunaweza kumpiga marufuku mtumiaji ikiwa tutaamini kwamba mtumiaji huyo anakiuka Masharti yetu ya Huduma.
Kwa taarifa zaidi kuhusu au mifano ya shughuli ambazo zinakiuka Masharti yetu ya Huduma, tafadhali kagua sehemu ya "Matumizi Yanayokubalika ya Huduma Zetu" kwenye Masharti yetu ya Huduma. Unaweza pia kupata maelezo zaidi kuhusu kupiga akaunti marufuku hapa.
Uwe makini na unachoshiriki
Tunakuhimiza ufikirie kwa makini kabla ya kuamua kushiriki kitu na unaowasiliana nao kwenye WhatsApp. Tafakari kama ungependa wengine waone kile ulichotuma.
Unaposhiriki soga, picha, video, faili au ujumbe wa sauti na mtu mwingine kwenye WhatsApp, atakuwa na nakala ya ujumbe huu. Atakuwa na uwezo wa kusambaza au kushiriki ujumbe huu na wengine akiamua kufanya hivyo. Kwa maelezo zaidi kuhusu kuangalia mara moja, soma makala haya.
Pia WhatsApp ina kipengele cha mahali ambacho unaweza kukitumia kushiriki mahali pako kwenye ujumbe wa WhatsApp. Unapaswa tu kushiriki mahali pako na watu unaowaamini pekee.
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia WhatsApp ipasavyo kwenye makala haya.
Vipengele vya usalama na ulinzi
Kwenye WhatsApp, tumetengeneza udhibiti fulani wa msingi ambao unaweza kuurekebisha kama inavyofaa kukusaidia kuwa salama.
Mipangilio ya faragha
Rekebisha mipangilio yako ya faragha ili udhibiti wanaoweza kuona taarifa zako. Unaweza kuweka maelezo yako ya mara ya mwisho kuonwa na kuwa mtandaoni, picha ya jalada, kuhusu au hali kati ya machaguo yafuatayo:
  • Kila mtu: Watumiaji wote wanaweza kuona picha ya jalada lako, kuhusu au hali.
  • Ninaowasiliana Nao: Watu walio kwenye kitabu chako cha anwani pekee ndiyo wanaweza kuona maelezo yako ya mara ya mwisho kuonwa na kuwa mtandaoni, picha ya jalada, kuhusu au hali.
  • Ninaowasiliana nao isipokuwa…: Unaowasiliana nao kwenye kitabu chako cha anwani, isipokuwa wale ambao hujawajumuisha, wanaweza kuona maelezo yako ya mara ya mwisho kuonwa na kuwa mtandaoni, picha ya jalada, kuhusu au hali.
  • Hakuna mtu: Hakuna mtu anaweza kuona maelezo yako ya mara ya mwisho kuonwa na kuwa mtandaoni, picha ya jalada, kuhusu au hali.
Kumbuka: Watumiaji uliowahifadhi kama anwani au ambao uliwatumia ujumbe hapo kabla wanaweza kuona mara yako ya mwisho kuona au kuwa mtandaoni.
Pata maelezo kuhusu mipangilio hii ya faragha kwenye: Android | iPhone
Taarifa za kusomwa
Unaweza pia kuzima taarifa za kusomwa. Ukizima taarifa za kusomwa, hutaweza kutuma au kupokea taarifa za kusomwa. Kumbuka taarifa za kusomwa hutumwa wakati wote kwa soga za kikundi, hata kama umezima chaguo hilo kwenye mipangilio ya faragha yako. Pata maelezo zaidi kuhusu taarifa za kusomwa kwenye Android, iPhone, au KaiOS.
Pata maelezo kuhusu mipangilio hii ya faragha kwenye: Android | iPhone
Kuzuia au kuripoti anwani na ujumbe
Tunakuhimiza uripoti kwetu maudhui na watumiaji wanaotatiza. Unaweza kudhibiti ni nani unatangamana naye kwa kuzuia anwani mahususi au kuripoti ujumbe au anwani kwenye WhatsApp. Unapopokea picha au video za kutazama mara moja, unaweza kuripoti akaunti hiyo papo hapo kwetu kwa kutumia sehemu ya kuangalilia maudhui. Fahamu kinachotokea unapotumia vipengele vya kuzuia na kuripoti na jinsi ya kufanya hivyo, kwenye makala haya.
Rasilimali za ziada za usalama
Ikiwa unahisi wewe au mtu mwingine yuko hatarini, tafadhali wasiliana na mtoa huduma za dharura mahali ulipo.
Ikiwa unaamini kuwa mtu fulani anataka kujiumiza na unajali usalama wake, tafadhali wasiliana na huduma za dharura za mahali ulipo au namba ya simu ya kuzuia kujitoa uhai.
Ukipokea au kukutana na maudhui yanayoonyesha kwamba mtoto ananyanyaswa au kudhulumiwa, tafadhali wasiliana na Kituo cha Taifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC). Unaweza pia kuripoti mtumiaji huyo. Pata maelezo zaidi kuhusu kuripoti hapa. Tafadhali usiweke picha yoyote ya skrini ya maudhui hayo kwenye ripoti yako.
Rasilimali zinazohusiana
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La