Â
Kuhusu uthibitishaji wa hatua mbili
Uthibitishaji wa hatua mbili ni kipengele cha hiari kinachoongeza usalama zaidi kwenye akaunti yako ya WhatsApp. Utaona skrini ya uhakiki wa hatua mbili baada ya kusajili nambari yako ya simu kwenye WhatsApp. Unaweza kupata maelezo ya jinsi ya kuwasha uthibitishaji wa hatua mbili kwenye makala haya.
Unapowasha uthibitishaji wa hatua mbili, una hiari ya kuweka anwani yako ya barua pepe. Kufanya hivyo huruhusu WhatsApp kukutumia barua pepe yenye kiungo cha kuweka upya PIN yako ikiwa utaisahau na pia kunakusaidia kulinda akaunti yako.
Ili kukusaidia ukumbuke PIN yako, WhatsApp itakuwa ikikuomba mara kwa mara uweke PIN yako. Hata hivyo, hakuna chaguo la kuzima hali hii bila kuzima kipengele cha uthibitishaji wa hatua mbili. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti mipangilio ya uthibitishaji wa hatua mbili kwenye makala haya.
Kumbuka: PIN ya uthibitishaji wa hatua mbili ni tofauti na msimbo wa usajili wa tarakimu 6 unaoupokea kupitia kwa SMS au kwa kupigiwa simu. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu usajili kwenye makala haya.
Rasilimali zinazohusiana:
Fahamu jinsi ya kulinda akaunti yako.