Â
Kuhusu Vyumba vya Messenger
Vyumba vya Messenger hukuwezesha kupiga simu na kutangamana na ndugu, marafiki na watu ambao mna mambo yanayowaunganisha. Kwa kutumia programu au tovuti ya Messenger, unaweza kuunda vyumba ambapo vikundi vikubwa vinaweza kujumuika ili kupiga soga ya video. Kisha unaweza kutuma viungo vya mwaliko kwa anwani na soga zako za kikundi kwenye WhatsApp. Pia marafiki wasio na akaunti ya Facebook au programu ya Messenger wanaweza kujiunga kwenye vyumba vya Messenger.
Njia za mkato za Vyumba vya Messenger hazipatikani tena kwenye WhatsApp. Messenger ni programu na tovuti tofauti. Unapounda chumba, utahitaji kuingia ukitumia akaunti yako ya Facebook. Kipengele cha Vyumba kipo nje ya WhatsApp na soga za video kwenye Vyumba vya Messenger hazilindwi kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho.
Mtumiaji yeyote wa WhatsApp unayeshiriki naye kiungo cha chumba anaweza kujiunga, kwa hivyo shiriki kiungo hiki na watu unaowaamini pekee. Inawezekana kwa mtu kusambaza kiungo kwa watu wengine. Ikiwa hivyo, pia watu hao wengine wanaweza kujiunga kwenye chumba, hata ikiwa hukuwatumia kiungo moja kwa moja.
Vyumba vya Messenger ni kipengele kinachomilikiwa na kuundwa na Messenger. Messenger na bidhaa zingine za Meta hazitumii lugha zote zinazotumika kwenye WhatsApp. Huenda ukaona baadhi ya ujumbe au viungo vilivyojazwa kiotomatiki kutoka Messenger katika lugha tofauti na iliyo kwenye simu au kompyuta yako. Unapotumia Vyumba vya Messenger au bidhaa zingine za Meta, unadhibitiwa na masharti na desturi za faragha za bidhaa husika. Kwa maelezo zaidi kuhusu Vyumba vya Messenger, tafadhali soma makala haya. Kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi WhatsApp hufanya kazi na Kampuni zingine za Meta, angalia Masharti ya Huduma na Sera yetu ya Faragha.