Jinsi ya kutumia vichujo vya orodha ya soga

Vichujio vya orodha ya soga hukuwezesha kutafuta kwenye orodha yako ya soga ili upate kwa haraka ujumbe mahususi kwenda na kutoka kwa wateja wako. Vichujio vya orodha ya soga hufanya iwe rahisi kupata vitu kama vile picha, GIF, viungo na nyaraka.
Kuweka kichujio cha orodha ya soga
  1. Fungua Programu ya WhatsApp Business > gusa Tafuta
    .
    • Kumbuka: Ikiwa kifaa chako ni iPhone, unaweza kuhitaji kutelezesha chini kwenye skrini kwanza.
  2. Chagua kichujio unachopenda kukitumia kutoka kwenye orodha kunjuzi.
Kumbuka: Vichujio haviwezi kufutwa au kubadilishwa.
Dokezo la Biashara: Kuna nyakati ambapo wateja wako wanaweza kukutumia picha zao wakitumia bidhaa zako. Ili uzipate picha hizi kwa haraka, tumia kichujio cha Picha kwenye orodha ya soga.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La