Jinsi ya kuwasha na kuzima nakala zilizofumbwa mwisho hadi mwisho

WhatsApp hutoa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwa ujumbe wote wa binafsi unaotuma na kupokea ili kuhakikisha kuwa wewe tu na mtu unayezungumza naye ndio mnaoweza kusoma au kusikiliza. Kupitia uwekaji nakala iliyofumbwa mwisho hadi mwisho, unaweza pia kuongeza safu ile ile ya ulinzi katika nakala ya soga zako kwenye iCloud na Hifadhi ya Google.
Kuwasha uwekaji wa nakala iliyofumbwa mwisho hadi mwisho
  1. Fungua Mipangilio.
  2. Gusa Soga > Nakala ya Soga > Ufumbaji wa nakala mwisho hadi mwisho.
  3. Gusa Washa, kisha ufuate vidokezo ili uunde nenosiri au ufunguo.
  4. Gusa Unda, kisha usubiri WhatsApp itayarishe nakala yako iliyofumbwa mwisho hadi mwisho. Huenda ukahitaji kuunganisha kwenye chanzo umeme.
Kumbuka: Hutaweza kurejesha nakala yako ikiwa utapoteza soga zako za WhatsApp na usahau nenosiri au ufunguo wako. WhatsApp haiwezi kuweka upya nenosiri lako au kurejesha nakala kwa niaba yako.
Kuzima uwekaji wa nakala iliyofumbwa mwisho hadi mwisho
  1. Fungua Mipangilio.
  2. Gusa Soga > Nakala ya Soga > Ufumbaji wa nakala mwisho hadi mwisho.
  3. Gusa Zima.
  4. Weka nenosiri lako.
  5. Thibitisha unataka kuzima nakala iliyofumbwa kwa kugusa Zima.
Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyokusanya na kuchakata data yako, pamoja na nakala iliyofumbwa mwishi hadi mwisho, tafadhali angalia Sera ya Faragha ya WhatsApp.
Rasilimali Zinazohusiana
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La