Kuhusu tarehe ya kuanza kutumika kwa sasisho la Januari 2021

Kitu gani kitafanyika tarehe ya kuanza kutumika?
Hakuna atakayefutiwa akaunti yake au kupoteza utendaji wa WhatsApp tarehe 15 Mei, 2021 kwa sababu ya sasisho hili.
Kitu gani kitafanyika baada ya tarehe ya kuanza kutumika?
Kwa kuzingatia kwamba idadi kubwa ya watumiaji ambao wameona sasisho wamelikubali, tutaendelea kuonyesha arifa katika WhatsApp ikiwa na maelezo zaidi kuhusu sasisho na kuwakumbusha wale ambao hawajapata fursa, wakague na kukubali. Kwa sasa hatuna mpango wa kufanya vikumbusho hivi viwe vya mara kwa mara na kupunguza utendaji wa programu.
Pia kutakuwa na fursa nyingine kwa wale ambao bado hawajakubali masasisho kufanya hivyo moja kwa moja kwenye programu. Kwa mfano, mtu anapojisajili kwenye WhatsApp au ikiwa mtu anataka kutumia kipengele ambacho kinahusiana na sasisho hili kwa mara kwa kwanza.
Unaweza kuhamisha historia ya soga zako kwenye Android au iPhone na kupakua ripoti ya akaunti yako.
  • Unaweza kuhamisha soga zako na kupakua ripoti ya akaunti yako pekee. Kama unataka msaada kupakua ripoti ya akaunti yako au kufuta akaunti yako, unaweza kuwasiliana nasi hapa.
WhatsApp haitafuta akaunti yako ikiwa hutakubali sasisho.
  • Pia kumbuka kwamba, sera yetu ya sasa inayohusu watumiaji wasiotumia akaunti zao itatumika.
  • Ikiwa ungependa kufuta akaunti yako kwenye Android, iPhone, au KaiOS, tunapendekeza utafakari uamuzi huo. Kufuta akaunti yako ni hatua ambayo hatuwezi kuibadilisha kwa vile hufuta historia yako ya ujumbe, hukuondoa kwenye vikundi vyako vyote vya WhatsApp na kufuta nakala ya soga zako za WhatsApp.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La