Jinsi ya kuweka au kuondoa nyota kwenye ujumbe

Android
iOS
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Mac
Kipengele cha ujumbe wenye nyota kinakuruhusu kuwekea ujumbe mahususi alama ili uweze kuurejelea baadaye.

Kuweka nyota kwenye ujumbe

 1. Fungua soga husika, kisha gusa na ushikilie ujumbe ambao ungependa kuuwekea nyota.
 2. Gusa
  star
  kwenye sehemu ya juu ya menyu.

Kuondoa nyota kwenye ujumbe

 1. Fungua soga husika, kisha uguse na ushikilie ujumbe wenye nyota.
 2. Gusa
  unstar
  kwenye sehemu ya juu ya menyu.
Kumbuka: Kuondoa nyota hakutafuta ujumbe.

Kuangalia orodha ya ujumbe ambao umewekea nyota

Ili uangalie orodha ya ujumbe wote wenye nyota kwenye akaunti yako, gusa
more options
> Ujumbe wenye nyota.

Je, hili linajibu swali lako?

Ndiyo
La