Jinsi ya kuhariri jalada lako

Unaweza kuhariri picha yako ya jalada, jina na taarifa kuhusu kwenye mipangilio ya WhatsApp.
Hariri picha yako ya jalada
 1. Fungua WhatsApp > gusa Hiari zaidi
  > Mipangilio.
 2. Gusa picha yako ya jalada.
 3. Gusa Matunzio kuchagua picha iliyopo au Kamera
  kupiga picha mpya.
 4. Kama una picha iliyopo sasa unaweza kuondoa picha.
Hariri jina lako la jalada
 1. Fungua WhatsApp > gusa Hiari zaidi
  > Mipangilio.
 2. Gusa picha yako ya jalada.
 3. Kwa Jina, gusa Hariri
  .
 4. Ingiza jina lako jipya.
  • Kikomo cha jina ni herufi 25.
  • Unaweza kuongeza emoji kwa kugusa Emoji
   .
 5. Gusa HIFADHI.
Jina lako la jalada litaonekana kwa watumiaji kwenye vikundi ambavyo hawajahifadhi maelezo yako ya mawasiliano kwenye vitabu vya anwani zao.
Hariri taarifa za kukuhusu
 1. Fungua WhatsApp > gusa Hiari zaidi
  > Mipangilio.
 2. Gusa picha yako ya jalada.
 3. Kwa Kuhusu, gusa Hariri
  .
 4. Unaweza kufanya mojawapo:
  • Chagua picha ya jalada.
  • Gusa Hariri
   kwa Sasa imewekwa kwa kubinafsisha taarifa zako. Kikomo cha maelezo ni herufi 139.
Taarifa zako haziwezi kuwa tupu.
Dokezo:
 • Unaweza kubadilisha mipangilio yako ya faragha ili kudhibiti nani anayeweza kuona picha ya jalada lako au taarifa kukuhusu.
 • Unaweza kuamua nani anayeweza kukuongeza kwenye vikundi kwa kubadilisha mipangilio yako ya faragha ya kikundi.
 • Kama ukimzuia mwasiliani, huyo mtu hataona sasisho zozote za picha ya jalada yako au taarifa.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La