Â
Kuhusu Code Verify
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Code Verify huongeza safu ya ziada ya usalama kwenye ufumbaji wa mwisho hadi mwisho wakati watu wanatumia WhatsApp kwenye wavuti.
Unapopakua kiendelezi cha kivinjari cha Code Verify kutoka kwenye duka rasmi la viendelezi kwa ajili ya Google Chrome, Mozilla Firefox na Microsoft Edge, huwa kinakagua kiotomatiki ikiwa unatumia toleo halisi na lisilobadilishwa la WhatsApp Web ili uweze kuwa na uhakika kwamba ujumbe wako ni kati yako na wapokeaji uliowakusudia wala si mtu mwingine. Kiendelezi kikigundua kuwa msimbo unaotumia kuendesha WhatsApp Web si sawa na msimbo ambao kila mtu anatumia, kiendelezi kitakuarifu ili uweze kuchukua hatua.
Jinsi ya kutumia kiendelezi cha Code Verify
Kwa hali bora ya utumiaji, hakikisha umebandika kiendelezi cha Code Verify kwenye upauzana wa kompyuta yako baada ya kukipakua ili uweze kuona kiendelezi na hali yake kwa urahisi. Kisha kiendelezi cha Code Verify kitafanya kazi kiotomatiki unapotumia WhatsApp Web (web.whatsapp.com). Kiendelezi kikiwa kimebandikwa kwenye upauzana wako na msimbo wa WhatsApp Web uthibitishwe kikamilifu, kiendelezi kitaonyesha alama ya tiki katika mduara wa kijani kwenye upauzana ili kuonyesha kwamba msimbo umethibitishwa kikamilifu.
Ikiwa kiendelezi hakiwezi kuthibitisha msimbo unaotumiwa, utaona mojawapo kati ya ujumbe tatu:
- Muda wa Mtandao Umeisha: Ikiwa ukurasa wako hauwezi kuthibitishwa kwa sababu muda umeisha katika mtandao wako, kiendelezi chako cha Code Verify kitaonyesha mduara wa rangi ya chungwa wenye alama ya kiulizi.
- Uwezekano wa Hatari Umegunduliwa: Ikiwa kiendelezi chako kimoja au zaidi kinatatiza uwezo wetu wa kuthibitisha ukurasa, kiendelezi chako cha Code Verify kitaonyesha mduara wa rangi ya chungwa wenye alama ya kiulizi.
- Imeshindwa Kuthibitisha: Ikiwa kiendelezi kitagundua kuwa msimbo unaoutumia kuendesha WhatsApp Web si sawa na msimbo unaotumiwa na kila mtu, aikoni ya Code Verify itageuka kuwa nyekundu na kuonyesha alama ya hisi.
Ukibofya aikoni ya kiendelezi cha Code Verify katika upauzana unapokuwa kijani, rangi ya chungwa au nyekundu, utaweza kuona maelezo zaidi. Tatizo likigunduliwa au hitilafu ya uthibitishaji ikitokea, bofya aikoni kufungua kitufe cha Pata Maelezo Zaidi. Bofya kwenye kitufe cha Pata Maelezo Zaidi ili uone jinsi ya kutatua tatizo. Pia utaweza kupakua chanzo cha msimbo ikiwa ungependa kuchunguza tatizo hilo zaidi. Soma zaidi kuhusu Code Verify kwenye makala haya.
Kumbuka:
- Kiendelezi cha kivinjari cha Uthibitishaji wa Msimbo huthibitisha tu kuwa msimbo msingi ulio kwenye WhatsApp Web ni sawa na msimbo ambao kila mtu anautumia. Kiendelezi hakitasoma wala kufikia ujumbe unaotuma au kupokea na hatutajua ikiwa umepakua kiendelezi chenyewe.
- Ufanisi wa kiendelezi cha Code Verify unaweza kutegemea kusimamisha au kuzima viendelezi vingine vya kivinjari unavyotumia.
- Kiendelezi cha kivinjari cha Code Verify huthibitisha msimbo kwa WhatsApp Web na hakina athari kwa WhatsApp Desktop.
- Kiendelezi hakihifadhi data yoyote, metadata au data ya mtumiaji na hakishiriki taarifa zozote na WhatsApp. Pia hakisomi au kufikia ujumbe unaotuma au kupokea.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kusakinisha kiendelezi cha kivinjari cha Code Verify
- Kwa nini ninaona hitilafu ya muda wa mtandao umeisha?
- Kwa nini ninaona onyo la kugunduliwa kwa uwezekano wa hatari ?
- Kwa nini ninaona onyo la imeshindwa kuthibitisha?