Jinsi ya kuondoka kwenye kikundi na kufuta vikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Unaweza kuwafutia washiriki wote kikundi ikiwa wewe ni msimamizi wa kikundi husika. Kabla ya kufuta kikundi ni sharti uondoe washiriki wote wa kikundi, kisha uondoke kwenye kikundi.
Ukifuta kikundi, hutakiona tena katika orodha ya soga zako na historia ya soga itafutwa kwenye simu yako. Washiriki wengine bado wataona kikundi kwenye orodha ya soga zao. Hata hivyo, hamna atakayeweza kutuma ujumbe.
Kuondoa washiriki wa kikundi
 1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubofye mada ya kikundi.
 2. Bofya Menyu
  karibu na jina la mshiriki > Ondoa > ONDOA.
Kuondoka kwenye kikundi
Ili ufute kikundi, ni sharti kwanza uondoke kwenye kikundi.
 1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubofye mada ya kikundi.
  • Au, elea juu ya kikundi kwenye orodha ya soga zako, kisha bofya Menyu
   .
 2. Bofya Ondoka kwenye kikundi
  > ONDOKA.
Kufuta kikundi
Baada ya kuondoka kwenye kikundi, utakuwa na chaguo la kufuta kikundi hicho.
 1. Fungua soga ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubofye mada ya kikundi.
  • Au, fanya kiashiria kielee juu ya kikundi kwenye orodha ya soga zako, kisha bofya Menyu
   .
 2. Bofya Futa kikundi
  > FUTA.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La