Kuhusu kupakia anwani

Upakiaji wa anwani ni kipengele cha hiari ambacho kinaturuhusu kuangalia ni nani kati ya walio kwenye kitabu cha anwani cha kifaa chako pia ni watumiaji wa WhatsApp. Pia, inamaanisha kuwa tunaweza kusasisha orodha ya anwani zako za WhatsApp wakati watu unaowasiliana nao ambao bado hawatumii WhatsApp watajisajili baadaye. Tunajali faragha yako na hatushiriki orodha yako ya anwani za mawasiliano na Meta Platforms Inc. au Kampuni nyingine za Meta kwa matumizi yao wenyewe, hata wakati wanatupatia huduma.
Unapotumia kipengele cha kupakia anwani na kuipa WhatsApp ruhusa ya kufikia kitabu cha anwani cha kifaa chako, WhatsApp itafikia na kupakia namba za simu kwenye kitabu chako cha anwani kwa kawaida kila siku, lakini hili linategemea vigezo kadhaa ikiwa ni pamoja na ni mara ngapi mtumiaji anatumia WhatsApp, ikiwa ni pamoja na watumiaji wa WhatsApp na watu wengine unaowasiliana nao. Hatukusanyi maelezo mengine yoyote ambayo yanaweza kuonekana katika kitabu cha anwani cha kifaa chako ikiwa ni pamoja na majina, anwani za barua pepe n.k.
Ikiwa mtu yeyote kati ya watu unaowasiliana nao bado hatumii WhatsApp, tunalinda faragha yake kwa kudhibiti namba ya simu kwa njia ambayo imeundwa ili kuzuia watu hao wasitambuliwe na WhatsApp. Tunafanya hivyo kwa kuunda thamani ya heshi ya kriptografia ya namba yake ya simu, na kisha kuifuta namba yenyewe. Kila thamani ya kriptografia huhifadhiwa kwenye seva za WhatsApp, ikiwa imeunganishwa na watumiaji wa WhatsApp ambao wamepakia namba husika za simu kabla ya kuzipa thamani ya heshi ili tuweze kukuunganisha kwa njia bora zaidi na watu hawa wanapojiunga na WhatsApp.
Vilevile, tunaunda heshi ya kriptografia inayowakilisha namba za simu zilizo katika kitabu cha anwani cha kifaa chako. Tunaitumia heshi hiyo kutambua na kupambana na matumizi mabaya ya upakiaji wa anwani. Kwa mfano, tunatathmini heshi ili kubaini ikiwa kumekuwa na mabadiliko yasiyo ya kawaida katika kitabu cha anwani. Hatua hii haijumuishi kufuatilia au kulinganisha namba za simu mahususi.
Unaweza kudhibiti kipengele cha kupakia anwani kutoka kwenye mipangilio iliyo katika kifaa chako. Ukichagua kutotumia Upakiaji wa Anwani bado unaweza kuwasiliana na watu walio na WhatsApp lakini utendakazi fulani utakuwa mdogo.
Soma zaidi kuhusu jinsi ya kutumia WhatsApp kwa umakini kwenye makala ya Kituo chetu cha Msaada.

Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La