Â
Tulisasisha Masharti yetu ya Huduma na Sera ya Faragha mnamo Januari 2021
Tulifanya mabadiliko kwenye Masharti yetu ya Huduma na Sera ya Faragha ambayo yanahusiana na kutuma ujumbe kati ya biashara na wateja wao kwenye WhatsApp na tukaanza kuisambaza Januari 2021. Kama sehemu ya sasisho hili, pia tunatoa maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyokusanya, kushiriki na kutumia data.
Ahadi yetu ya kulinda faragha yako haikubadilika. Mawasiliano yako ya binafsi bado yanalindwa kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, hii ina maana kwamba hakuna mtu nje ya soga zako, ikiwa ni pamoja na WhatsApp au Meta, anaweza kuyasoma wala kuyasikiliza.
Ni jukumu letu kufafanua masasisho haya kwa uwazi. Haya ndiyo baadhi ya mambo unayofaa kuyajua:
Kitu gani kimebadilika
Unaweza kuwasiliana na biashara zaidi kwenye WhatsApp ili mambo yafanyike kwa haraka zaidi ikilinganishwa na kupiga simu au kutumia barua pepe. Utendaji huu ni wa hiari kabisa.
Kila siku, mamilioni ya watu hutumia WhatsApp kuwasiliana na biashara, ziwe kubwa au ndogo. Unaweza kuwasiliana na biashara ili kuuliza maswali, kununua au kupata taarifa. Ni uamuzi wako ikiwa unataka kupiga soga na biashara kwenye WhatsApp, unaweza kuzizuia au kuziondoa kwenye orodha yako ya anwani.
Biashara kubwa, kama vile mashirika ya ndege au maduka makubwa, zinaweza kupokea maelfu ya mawasiliano kutoka kwa wateja wao kwa wakati mmoja - wakiomba taarifa kuhusu ndege au kufuatilia bidhaa waliyoagiza. Ili kuhakikisha kwamba majibu yanatolewa haraka, biashara hizi zinaweza kutumia Meta kuwa mtoa huduma za teknolojia ya kudhibiti baadhi ya majibu kwa niaba yao. Tutaweka alama waziwazi kwenye soga ili ufahamu hali hii inapotokea.
Tulitoa maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyokusanya, kushiriki na kutumia data.
Mabadiliko kwenye Sera yetu ya Faragha yanakupa maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyodhibiti taarifa zako. Tumeongeza maelezo zaidi kwenye sehemu fulani za Sera yetu ya Faragha na pia tumeongeza sehemu mpya. Pia tumerahisisha mpangilio wa Sera ya Faragha na kurahisisha utumiaji na usogezaji.
Unaweza kupakua ripoti ya taarifa na mipangilio ya akaunti yako ya WhatsApp hapa.
Kisichobadilika
Faragha na usalama wa soga za binafsi kati yako na familia na marafiki haitabadilika kamwe.
WhatsApp wala Meta haziwezi kuona maudhui unayoshiriki na familia na marafiki zako, hayo ni pamoja na ujumbe na simu, viambatisho mnavyotumiana au unaposhiriki mahali ulipo. Hatuweki kumbukumbu ya watu wowote wanaotumiwa ujumbe au kupigiwa simu na WhatsApp haishiriki anwani zako na Meta.
Udhibiti ni wako. Ni wewe unaamua kama unataka au hutaki kushiriki namba yako na biashara, pia unaweza kuzuia biashara wakati wowote.
WhatsApp haiwezi kuipa biashara nambari yako, pia sera zetu zinakataza biashara kuwasiliana na wewe kwenye WhatsApp kabla ya kupokea idhini yako kufanya hivyo.
Vipengele vyetu vya ziada vya faragha, kama vile kufanya ujumbe wako utoweke au kudhibiti anayeweza kukuongeza kwenye vikundi, hukupa safu ya ziada ya faragha.
Kukubali Masharti mapya ya Huduma hakupanui uwezo wa WhatsApp kushiriki data ya watumiaji na kampuni yake kuu, Meta.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali kagua masharti yetu na sera yetu ya faragha. Pia unaweza kupata majibu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara hapa.