Â
Jinsi ya kuhifadhi historia yako ya soga
Android
Soga zako za WhatsApp huchelezwa kiotomatiki na kuhifadhiwa kila siku kwenye kumbukumbu ya simu yako. Kutegemea mipangilio yako, pia unaweza kucheleza soga zako za WhatsApp mara kwa mara kwenye Hifadhi ya Google. Ukiondoa WhatsApp kwenye simu yako, lakini hutaki kupoteza ujumbe wowote, hakikisha unacheleza soga zako kabla ya kuondoa programu.
Kucheleza soga
Nenda kwenye WhatsApp > gusa Chaguo zaidi
> Mipangilio > Soga > Chelezo ya soga > CHELEZA.

Kuhamisha historia ya soga
Unaweza kutumia kipengele cha kuhamisha soga ili uhamishe nakala ya historia ya soga kutoka kwenye soga ya binafsi au ya kikundi.
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Gusa Chaguo zaidi> Zaidi > Hamisha soga.
- Chagua ikiwa unataka kuhamisha pamoja na midia au bila midia.
Barua pepe itatungwa huku historia yako ya soga ikiwa imeambatishwa kama hati ya .txt.
Kumbuka:
- Ikiwa upo Ujerumani, huenda itakubidi usasishe WhatsApp kabla ya kutumia kipengele cha kuhamisha.
- Ukichagua kuambatisha midia, midia ya hivi karibuni zaidi yatawekwa kwenye viambatisho.
- Unapohamisha pamoja na midia, unaweza kutuma hadi ujumbe 10,000 wa hivi karibuni. Bila midia, unaweza kutuma hadi ujumbe 40,000. Vikwazo hivi kwa sababu ya kima cha juu kinachoruhusiwa kwenye barua pepe.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kurejesha historia yako ya soga
- Jinsi ya kucheleza kwenye Hifadhi ya Google