Kuhusu kubadilisha namba ya simu

Kipengele cha kubadilisha namba kinakuruhusu kubadilisha namba ya simu inayohusiana na akaunti yako ya WhatsApp. Kubadilisha namba yako ya simu kwenye WhatsApp kutasababisha yafuatayo:
  • Kuhamisha maelezo ya akaunti yako, ikiwa ni pamoja na picha yako ya jalada, jina, maelezo ya kuhusu, soga za binafsi, soga za kikundi na mipangilio kutoka kwenye namba yako ya zamani ya simu kwenda kwenye namba yako mpya ya simu.
  • Kufuta akaunti yako ya WhatsApp inayohusishwa na namba yako ya zamani ya simu, kwa hivyo unaowasiliana nao hawataweza tena kuona namba yako ya simu ya zamani kwenye orodha ya anwani zao za WhatsApp.
Unaweza kuchagua ikiwa ungependa kuwaarifu unaowasiliana nao kuhusu mabadiliko ya namba yako ya simu. Vikundi vyako vya soga vitaarifiwa unapobadilisha namba yako ya simu bila kuzingatia ikiwa umechagua kuwaarifu unaowasiliana nao. Tunapendekeza uwajulishe unaowasiliana nao kuhusu namba yako mpya ya simu kabla ya kubadilisha namba ya simu. Waombe wafanye mabadiliko yoyote muhimu kwenye kitabu cha anwani cha simu zao.
Kumbuka: Ikiwa utabadilisha namba yako ya simu na uendelee kutumia simu ileile kwa namba mpya ya simu, utaendelea kupata historia ya soga zako kwenye simu yako.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La