Kuhusu kuunganisha WhatsApp Business, Facebook na Instagram

Ili uwape wateja wako njia nyingine ya kuwasiliana na biashara yako, unaweza kuunganisha akaunti yako ya WhatsApp Business na Ukurasa wa Facebook na/au Jalada la Instagram. Ukiwa umeunganisha Ukurasa wa Facebook au Jalada lako la Instagram na akaunti yako ya WhatsApp Business, namba yako itaonekana kama chaguo la kuwasiliana kwenye Ukurasa wa Facebook na/au Jalada la Instagram iliyounganishwa. Mteja akigusa chaguo hili la kuwasiliana, ataweza kukutumia ujumbe moja kwa moja kwenye WhatsApp.
Baada ya kuunganisha, Ukurasa wako wa Facebook husawazisha taarifa za biashara kiotomatiki kwenye akaunti yako ya WhatsApp Business.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La