Kuhusu kuunganisha WhatsApp Business kwenye Facebook na Instagram

Android
iOS
Unaweza kuunganisha akaunti yako ya WhatsApp Business na Ukurasa wa Facebook au jalada lako la Instagram Business la biashara.
Baada ya kuunganisha, namba ya akaunti yako ya WhatsApp Business pia itaonekana kama chaguo la mawasiliano kwenye Ukurasa wa Facebook au jalada la Instagram Business lililounganishwa. Mteja anapogusa chaguo hili la kuwasiliana, ataweza kukutumia ujumbe moja kwa moja kwenye WhatsApp.
  Kwa kuunganisha Ukurasa wa Facebook au jalada la Instagram Business, utaweza:
 • Wasaidie wateja watarajiwa wapate maelezo zaidi kuhusu biashara yako
 • Tumia utambulisho wa biashara (ukurasa wa Facebook au jalada la IG Business) ili uunde matangazo yanayoonekana kwenye Facebook na Instagram, moja kwa moja kutoka kwenye programu ya Whatsapp Business. Boresha mipangilio ya mtangazaji na ulipie tangazo lako kwa urahisi ukitumia njia ya kulipa unayotumia kwenye Facebook au Instagram.
Kumbuka: Machapisho machache ya mwisho kwenye Ukurasa wako wa Facebook au jalada lako la Instagram Business pia yataonekana kwenye jalada lako la WhatsApp Business. Huenda kipengele hiki bado hakipatikani kwenye eneo lako.
Kuna njia kadhaa za kudhibiti akaunti zako zilizounganishwa:
Android:
 • Ikiwa hungependa viungo vya machapisho na machapisho ya Ukurasa wako wa Facebook au jalada la Instagram Business yaonekane kwenye jalada lako la WhatsApp Business, gusa
  shopping
  > Facebook na Instagram. Chagua Ukurasa wako wa Facebook au jalada la Instagram kisha uzime Onyesha kwenye jalada.
 • Ikiwa hungependa machapisho ya Ukurasa wako wa Facebook au jalada la Instagram Business yaonekane kwenye matokeo ya utafutaji kwenye saraka ya Biashara, utahitaji kutenganisha akaunti zako.
 • Ikiwa ungependa kutenganisha ukurasa wako wa Facebook au jalada lako la Instagram Business kutoka kwenye akaunti yako ya WhatsApp, gusa
  shopping
  > Facebook na Instagram. Chagua Ukurasa wako wa Facebook au jalada lako la Instagram. Kwenye kona ya juu upande wa kulia, gusa Ondoa WhatsApp.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La