Jinsi ya kupiga simu ya sauti

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Mac
Simu ya sauti hukuruhusu kuwapigia unaowasiliana nao simu bila malipo ukitumia WhatsApp, hata ikiwa upo nchi nyingine. Kipengele cha kupiga simu ya sauti hutumia muunganisho wa intaneti wa simu yako badala ya kifurushi chako cha dakika za maongezi. Gharama za data zinaweza kutumika.
Unaweza kupiga simu ya WhatsApp kwenye simu ya KaiOS inayotumia toleo la KaiOS la:
  • 2.5.1.2 au jipya zaidi
  • 2.5.2.2 au jipya zaidi
  • 2.5.3 au jipya zaidi
Kupiga simu ya sauti
Kupiga simu kwenye kichupo cha Soga
  1. Kwenye kichupo cha Soga, chagua anwani ambayo ungependa kupigia simu.
  2. Bonyeza Chaguo > Simu ya sauti.
Wakati wa simu, unaweza kuzima au kuwasha maikrofoni yako kwa kubonyeza Zima. Ili ukate simu, bonyeza Kata.
Kupiga simu kwenye kichupo cha Simu
  1. Kwenye kichupo cha Simu, bonyeza Simu Mpya.
  2. Chagua anwani ambayo ungependa kupigia simu ya sauti.
  3. Bonyeza SIMU.
Kujibu simu
Ukipokea simu ya sauti ya WhatsApp, unaweza kufanya yafuatayo:
  • Kubali ili upokee simu.
  • Kata ili ukate simu.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La