Â
Jinsi ya kupiga simu ya sauti
Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Simu ya sauti hukuruhusu kuwapigia simu unaowasiliana nao bila malipo kwa kutumia WhatsApp, hata ikiwa upo nchi nyingine. Kupiga simu ya sauti kunatumia muunganisho wa intaneti wa simu yako badala ya dakika za mpango wako wa simu ya mkononi. Unaweza kutozwa ada za data.
Kupiga simu ya sauti
- Fungua soga ya binafsi na mtu unayetaka kumpigia simu.
- Gusa Simu ya sauti.
Vinginevyo, fungua WhatsApp, kisha uguse kichupo cha SIMU > Piga simu mpya
. Tafuta mtu unayetaka kumpigia simu ya sauti, kisha uguse Piga simu ya sauti
.


Kupokea simu ya sauti
Ikiwa simu yako imefungwa, utaona skrini ya Simu ya sauti ya WhatsApp inaingia wakati mtu fulani anapokupigia simu, utaweza:
- Telezesha juu ili upokeeili ujibu simu.
- Telezesha juu ili ukateili ukate simu.
- Telezesha juu ili ujibuili ukatae simu na kutuma ujumbe wa haraka.
Ikiwa simu yako haijafungwa, utaona ibukizi ya Simu ya sauti inayoingia wakati mtu fulani anapokupigia simu, ambapo unaweza kugusa Kataa au Jibu.
Kubadilisha kati ya simu ya sauti na simu ya video
Kubadilisha kutoka kwa simu ya sauti kwenda kwa simu ya video
- Unapokuwa katika simu ya sauti, gusa Simu ya video> BADILISHA.
- Mtumiaji unayempigia simu ataona ombi la kubadilisha kuwa simu ya video na anaweza kukubali au kukataa kubadilisha.
Kubadili kutoka simu ya video kuwa simu ya sauti
- Ukiwa kwenye simu ya video, gusa Zima video, hatua itakayomjulisha unayewasiliana naye kuwa unampigia simu ya video.
- Baada ya mtu unayewasiliana kuzima video yake, simu itabadilishwa na kuwa simu ya sauti.
Kumbuka:
- Hakikisha kwamba wewe na unaowasiliana nao mna muunganisho wa Intaneti ulio imara wakati mnapiga au kupokea simu za video za kikundi. Ubora wa simu utategemea mwasiliani mwenye muunganisho dhaifu.
- Huwezi kufikia namba za huduma za dharura kupitia WhatsApp, kama vile 911 nchini Marekani. Kupiga simu za dharura, unapaswa kufanya mipango ya mawasiliano mbadala.
Rasilimali zinazohusiana: