Jinsi ya kupiga simu ya sauti

Android
iOS
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Mac
Simu ya sauti hukuruhusu kuwapigia watu unaowasiliana nao simu bila malipo kutumia WhatsApp Desktop, hata ikiwa wapo nchi nyingine. Simu ya sauti hutumia muunganisho wako wa intaneti. Unaweza kupiga simu kwenye kompyuta inayotumia mfumo wa Windows 10 64-bit toleo la 1903 au matoleo mapya na toleo la macOS 11 au matoleo mapya.
Kupiga simu kupitia kompyuta
Ili upige au upokee simu za sauti kwenye WhatsApp Desktop:
 • Utahitaji muunganisho wa intaneti unaofanya kazi kwenye kompyuta na simu yako.
 • WhatsApp inahitaji kufikia maikrofoni ya kompyuta yako.
 • Utahitaji kuwa na kifaa cha kutoa sauti, maikrofoni iliyounganishwa kwenye kompyuta yako kwa ajili ya simu.
Kumbuka: Tumia vipokea sauti vinavyobanwa kichwani kwa sauti bora. Kutumia vifaa tofauti kwa ajili ya maikrofoni na spika kunaweza kusababisha mwangwi.
Kupiga simu ya sauti
 1. Fungua soga ya binafsi kati yako na anwani ambayo ungependa kupigia simu.
 2. Bofya aikoni ya Simu ya sauti.
Wakati wa simu, unaweza kuzima au kuwasha maikrofoni yako kwa kubofya aikoni ya Maikrofoni. Simu inapokamilika, bofya Kata simu.
Kupokea simu ya sauti
Ikiwa una simu inayoingia, unaweza kubofya:
 • Kubali ili upokee simu.
 • Kata ili ukate simu.
 • Puuza au x ili upuuze simu.
Kubadilisha kati ya simu ya sauti na simu ya video
Ukiwa kwenye simu ya sauti na mtu unayewasiliana naye, unaweza kuomba kubadilisha ili mtumie simu ya video. Mtu unayempigia simu ya sauti anaweza kubofya SAWA au Badilisha ili kubadilisha simu au Ghairi ili kuikata.
 1. Wekelea kiashiria kwenye aikoni ya Kamera wakati wa simu.
 2. Bofya aikoni ya Kamera.
 3. Simu ya sauti itabadilika kuwa simu ya video ikiwa unayewasiliana naye atakubali kubadili.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La