Kuhusu mifumo ya uendeshaji inayotumika

Kwa sasa, mfumo wetu unaweza kutumia na tunapendekeza utumiaji wa vifaa vifuatavyo:
  • Android inayotumia mfumo wa uendeshaji wa toleo la OS 5.0 na matoleo mapya zaidi
  • iPhone inayotumia mfumo wa uendeshaji wa toleo la iOS 12 na matoleo ya baadaye
  • Toleo la KaiOS 2.5.0 na matoleo ya baadaye, ikiwa ni pamoja na JioPhone na JioPhone 2
Mara tu ukiwa na mojawapo ya vifaa hivi, sakinisha WhatsApp kisha usajili namba yako ya simu.
Kumbuka: Simu yako lazima iwe na uwezo wa kupokea SMS au simu wakati wa mchakato wa uthibitishaji. Haturuhusu uanzishaji wa akaunti mpya kwenye vifaa vinavyotumia WiFi pekee.
Jinsi tunavyochagua mifumo ya kutumia
Vifaa na programu hubadilika mara kwa mara, kwa hivyo huwa tunakagua ni mifumo gani ya uendeshaji tunayoweza kutumia na kufanya masasisho.
Kila mwaka tunaangalia ni vifaa na programu ambazo ni za zamani zaidi na zina watumiaji wachache zaidi. Vifaa hivyo pia huenda visiwe na masasisho ya hivi karibuni ya usalama au huenda havina utendaji unaohitajika ili kuendesha WhatsApp.
Kitakachotokea ikiwa mfumo wako wa uendeshaji hautumiki tena
Kabla hatujaacha kutumia mfumo wako wa uendeshaji, utaarifiwa kwenye WhatsApp na kukumbushwa mara kadhaa ili uboreshe.
Tutasasisha ukurasa huu mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa tumeorodhesha mifumo ya hivi karibuni ya uendeshaji tunayotumia.
Rasilimali zinazohusiana:
Kuhusu vifaa vinavyotumika
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La