Kuhusu mifumo ya uendeshaji inayotumika

Kwa sasa, mfumo wetu unaweza kutumia na tunapendekeza utumiaji wa vifaa vifuatavyo:
  • Android inayotumia mfumo wa uendeshaji wa toleo la OS 4.1 au matoleo ya baadaye
  • iPhone inayotumia mfumo wa uendeshaji wa toleo la iOS 12 na matoleo ya baadaye
  • Toleo la KaiOS 2.5.0 na matoleo ya baadaye, ikiwa ni pamoja na JioPhone na JioPhone 2
Mara tu ukiwa na mojawapo ya vifaa hivi, sakinisha WhatsApp kisha usajili namba yako ya simu.
Kumbuka:
  • Kuanzia tarehe 24 Oktoba, 2023 toleo la Android OS la 5.0 na matoleo mapya zaidi ndio yatakayotumika.
  • Simu yako lazima iwe na uwezo wa kupokea SMS au simu wakati wa mchakato wa uthibitishaji. Haturuhusu uanzishaji wa akaunti mpya kwenye vifaa vinavyotumia WiFi pekee.
Jinsi tunavyochagua mifumo ya kutumia
Vifaa na programu hubadilika mara kwa mara, kwa hivyo huwa tunakagua ni mifumo gani ya uendeshaji tunayoweza kutumia na kufanya masasisho.
Ili kuchagua ni wapi hatutaendelea kutumika, kila mwaka, sawa na kampuni zingine za teknolojia, huwa tunaangalia ni vifaa na programu zipi ni za zamani sana na zina idadi ndogo zaidi ya watu ambao bado wanazitumia. Vifaa hivyo pia huenda visiwe na masasisho ya hivi karibuni ya usalama au huenda havina utendaji unaohitajika ili kuendesha WhatsApp.
Kitakachotokea ikiwa mfumo wako wa uendeshaji hautumiki tena
Kabla hatujaacha kutumia mfumo wako wa uendeshaji, utaarifiwa moja kwa moja kwenye WhatsApp mapema na kukumbushwa mara kadhaa ili uboreshe.
Tutasasisha ukurasa huu mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa tumeorodhesha mifumo ya hivi karibuni ya uendeshaji tunayotumia.
Rasilimali zinazohusiana:
Kuhusu vifaa vinavyotumika
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La