Faragha na usalama kwa ujumbe wa kibiashara

Utumaji Ujumbe wa Kibiashara
Kila ujumbe wa WhatsApp hulindwa na itifaki ile ile ya ufumbaji wa Signal ambayo hudumisha usalama wa ujumbe kabla haujatoka kwenye kifaa chako. Unapotuma ujumbe kwenda kwenye akaunti ya WhatsApp ya biashara, ujumbe wako hufikishwa kwa usalama kwenye sehemu iliyochaguliwa na biashara hiyo.
WhatsApp inachukulia kwamba soga kati yako na biashara zinazotumia programu ya WhatsApp Business au zinazosimamia na kujihifadhia ujumbe wa wateja huwa zimefumbwa mwisho hadi mwisho. Mara tu ujumbe ukishapokelewa, utakuwa chini ya desturi za faragha za biashara husika. Biashara hiyo inaweza kuwapa idadi fulani ya wafanyakazi, au hata mashirika mengine, jukumu la kuchakata na kujibu ujumbe.
Baadhi ya biashara1 zitaweza kuchagua kampuni kuu ya WhatsApp, ambayo ni Meta, katika kuhifadhi ujumbe kwa usalama na kujibu wateja. Ingawa Facebook haitaonyesha ujumbe kati yako na biashara kwenye akaunti yoyote ya binafsi ya Facebook wala kutumia ujumbe wako kiotomatiki kubaini matangazo unayoyaona, biashara zitaweza kutumia soga zinazopokea kwa madhumuni yao ya matangazo, ambayo yanaweza kuwa ni pamoja na matangazo kwenye Meta. Unaweza kuwasiliana na biashara husika wakati wowote ili upate maelezo zaidi kuhusu desturi zake za faragha.
Kumbuka: Hali ya ufumbaji wa mwisho hadi mwisho hauwezi kubadilika bila badiliko hilo kuonekana kwa mtumiaji. Kwa maelezo zaidi kuhusu ni soga zipi hufumbwa mwisho hadi mwisho, tafadhali soma waraka wetu rasmi.
Udhibiti ni wako
WhatsApp inataka kuhakikisha kuwa unaelewa kinachofanyika kwa ujumbe wako. Ikiwa hutaki kupokea ujumbe kutoka kwa mtu au biashara, unaweza kumzuia moja kwa moja kwenye soga au umfute kutoka kwenye orodha ya unaowasiliana nao. Tunataka kuhakikisha kuwa unaelewa jinsi ujumbe wako unavyoshughulikiwa na kwamba una chaguo unazohitaji kufanya uamuzi unaokufaa.
1Mwaka wa 2021.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La