Jinsi ya kuzuia na kuripoti anwani

Android
iPhone
KaiOS
Unaweza kuacha kupokea ujumbe na simu kutoka kwa watumiaji fulani kwa kuwazuia. Pia, unaweza kuwaripoti kama unadhani kuwa wanatuma maudhui yanayotatiza au taka.
Ikiwa unahisi wewe au mtu mwingine yeyote yuko hatarini, tafadhali wasiliana mtoa huduma za dharura mahali ulipo.
Kuzuia anwani
 1. Bonyeza Chaguo > Mipangilio > Akaunti > Faragha > Anwani zilizozuiwa > Ongeza mpya...
 2. Tafuta au chagua mtumiaji unayetaka kumzuia.
 3. Bonyeza ZUIA.
Dokezo:
 • Ukibadili namba yako ya simu na utumie akaunti ileile ya WhatsApp, anwani ulizozuia zitabaki zikiwa zimezuiwa. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia kipengele cha kubadili namba kwenye makala haya.
  • Ukifungua akaunti mpya ya WhatsApp, utahitaji kuzuia anwani hizo tena.
Unaweza kutumia mbinu hizi mbadala za kuzuia mtumiaji:
 • Chagua soga kati yako na anwani kwenye orodha yako ya soga, kisha ubonyeze Chaguo > Angalia anwani > Zuia > Zuia.
 • Fungua soga kati yako na anwani, kisha ubonyeze Chaguo > Angalia anwani > Zuia > Zuia.
Kuzuia nambari ya simu usiyoijua
Ili kuzuia nambari ya simu usiyoijua, una chaguo mbili:
 • Chagua soga kati yako na namba ya simu usiyoijua kwenye orodha yako ya soga, kisha ubonyeze Chaguo > Angalia anwani > Zuia > Zuia.
 • Fungua soga kati yako na namba ya simu usiyoijua, kisha ubonyeze Chaguo > Angalia anwani > Zuia > Zuia.
Kumbuka:
 • Watumiaji waliozuiwa hawataweza tena kukupigia simu au kukutumia ujumbe.
 • Mara yako ya mwisho kuonwa, kuwa mtandaoni na mabadiliko yoyote unayofanya kwenye picha yako ya jalada hayataonekana tena kwa watumiaji uliowazuia.
 • Kumzuia mtu hakutamwondoa kwenye orodha yako ya watumiaji, wala hakutakuondoa kwenye orodha iliyo kwenye simu ya mtumiaji huyu. Ili ufute mtu, lazima umfute kutoka kwenye kitabu cha anwani cha simu yako.
 • Kama una wasiwasi ikiwa mtu ambaye umezuia atajua kuwa umemzuia, tafadhali soma makala haya.
Kuruhusu mtumiaji
 1. Bonyeza Chaguo > Mipangilio > Akaunti > Faragha > Anwani zilizozuiwa.
 2. Chagua mtumiaji unayetaka kumruhusu.
 3. Bonyeza RUHUSU.
Unaweza kutumia mbinu hizi mbadala za kumruhusu mtumiaji:
 • Chagua soga kati yako na anwani kwenye orodha yako ya soga, kisha ubonyeze Chaguo > Angalia anwani > Ruhusu.
 • Fungua soga kati yako na anwani, kisha ubonyeze Chaguo > Angalia anwani > Ruhusu.
Kumbuka:
 • Ukimruhusu mtumiaji, hutapokea ujumbe wowote uliotumwa au simu zilizopigwa wakati alikuwa amezuiliwa.
 • Ukimruhusu mtumiaji au nambari ya simu ambayo ulikuwa hujaihifadhi kwenye kitabu cha anwani cha simu yako, hutaweza kumrejesha mtumiaji huyo au nambari ya simu kwenye simu yako.
Kuripoti mtumiaji
 1. Fungua soga na mtumiaji unayetaka kumripoti.
 2. Bonyeza Chaguo kisha uchague Angalia anwani.
 3. Bonyeza Ripoti na uzuie au Ripoti tu.
Kumbuka: WhatsApp itapokea ujumbe tano uliotumwa kwako na mtumiaji au kikundi unachoripoti na hawatajulishwa. WhatsApp pia hupokea Kitambulisho cha kikundi kilichoripotiwa au cha mtumiaji, taarifa ya wakati ujumbe huo ulitumwa na aina ya ujumbe uliotumwa (picha, video, maandishi, n.k.).
Kuripoti picha au video ya kutazama mara moja
 1. Fungua picha au video ya kutazama mara moja.
 2. Bonyeza Chaguo kwenye sehemu ya kona ya chini.
 3. Bonyeza Ripoti.
Kupata maelezo zaidi kuhusu kipengele cha kuangalia mara moja, soma makala haya.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La