Â
Jinsi ya kuzuia na kuripoti anwani
Android
iPhone
KaiOS
Unaweza kusitisha kupokea ujumbe, simu na masasisho ya hali kutoka kwenye anwani fulani kwa kuzizuia. Pia, unaweza kuwaripoti kama unadhani kuwa wanatuma maudhui yanayotatiza au taka.
Ikiwa unahisi wewe au mtu mwingine yeyote yuko hatarini, tafadhali wasiliana mtoa huduma za dharura mahali ulipo.
Kuzuia anwani
- Fungua Mipangilio ya WhatsApp > Faragha > Anwani zilizozuiwa > Ongeza Mpya...
- Tafuta mtumiaji unayetaka kumzuia, kisha gusa anwani yake.
Kumbuka:
- Ukibadili namba yako ya simu na utumie akaunti ileile ya WhatsApp, anwani ulizozuia zitabaki zikiwa zimezuiwa. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia kipengele cha kubadili namba kwenye makala haya.
- Ukifungua akaunti mpya ya WhatsApp, utahitaji kuzuia anwani hizo tena.
Njia zaidi za kuzuia anwani:
- Fungua soga kati yako na anwani, kisha uguse jina la anwani > Zuia Anwani > Zuia au Ripoti Anwani > Ripoti na Uzuie b>.
- Kwenye kichupo chako cha Soga, telezesha soga kushoto, kisha uguse Zaidi > Maelezo ya Anwani > Zuia Anwani > Zuia au Ripoti Anwani > Ripoti na Uzuie.
Kuzuia namba ya simu usiyoijua
Kuzuia namba ya simu usiyoijua, una chaguo mbili:
- Ikiwa hii ndiyo mara yako ya kwanza kuwasiliana na namba hiyo ya simu, unaweza kufungua soga kisha uguse Zuia > Zuia.
- Fungua soga kati yako na namba hiyo ya simu, kisha uguse namba ya simu > Zuia Anwani > Zuia au Ripoti Anwani > Ripoti na Uzuie.
Kumbuka:
- Unapogusa Ripoti na Uzuie utaripoti na kuzuia namba hiyo.
- Watumiaji uliowazuia hawataweza tena kukupigia simu au kukutumia ujumbe.
- Mara yako ya mwisho kuonwa, kuwa mtandaoni, masasisho ya hali na mabadiliko yoyote unayofanya kwenye picha yako ya jalada hayataonekana tena kwa anwani ambazo umezuia.
- Kumzuia mtu hakutamwondoa kwenye orodha yako ya anwani, wala hakutakuondoa kwenye orodha iliyo kwenye simu ya mtumiaji huyo. Ili ufute mtu, lazima umfute kutoka kwenye kitabu cha anwani cha simu yako.
- Ikiwa una wasiwasi iwapo mtu uliyemzuia atajua kuwa umefanya hivyo, tafadhali soma makala haya.
Kuruhusu anwani
- Gusa Mipangilio > Faragha > Anwani ulizozuia.
- Telezesha kushoto kwenye jina la anwani.
- Au, gusa Hariri > aikoni ya alama ya nyekundu ya kutoa.
- Gusa Ruhusu.
Njia zaidi za kuruhusu anwani:
- Fungua soga kati yako na anwani, kisha uguse jina la anwani > Ruhusu Anwani.
- Telezesha kushoto kwenye soga kati yako na anwani kwenye kichupo chako cha Soga, kisha uguse Zaidi > Maelezo ya Anwani > Ruhusu Anwani.
Kumbuka: Ukiruhusu anwani, hutapokea ujumbe, simu na masasisho yoyote ya hali ambayo anwani hiyo ilituma wakati ilipokuwa imezuiwa.
Kuripoti anwani
- Fungua soga kati yako na anwani unayotaka kuripoti.
- Gusa jina la anwani, kisha uguse Ripoti Anwani.
- Gusa Ripoti na Uzuie.
Kumbuka: WhatsApp hupokea ujumbe tano uliotumwa kwako na mtumiaji au kikundi unachoripoti na hawatajulishwa. WhatsApp pia hupokea Kitambulisho cha kikundi au mtumiaji, maelezo ya wakati ambapo ujumbe ulitumwa na aina ya ujumbe uliotumwa (kwa mfano, picha, video, maandishi).
Pia, unaweza kuchagua kuripoti akaunti kwa kubonyeza ujumbe mmoja kwa muda.
- Bonyeza ujumbe wa mtu kwa muda. Fungua menyu ya maudhui kisha uguse Ripoti.
- Arifa ya uthibitishaji itaonyeshwa kabla ya kutuma ripoti. Unaweza pia kumzuia na kumripoti mtumiaji huyo.
Kuripoti picha au video ya kuangalia mara moja
- Fungua picha au video ya kuangalia mara moja.
- Gusa Zaidikwenye sehemu ya kona ya chini.
- Gusa Ripoti Anwani.
Kupata maelezo zaidi kuhusu kipengele cha kuangalia mara moja, soma makala haya.