Akaunti zilizoibiwa

Kuhusu akaunti zilizoibiwa
Kamwe usiwape watu wengine msimbo wako wa uthibitisho wa SMS kutoka WhatsApp, hata kama ni marafiki au familia yako. Ikiwa umehadaiwa ukashiriki msimbo wako na ukapoteza ufikiaji wa akaunti yako ya WhatsApp, soma maagizo hapa chini ili urejeshe akaunti yako.
Ikiwa unashuku kuwa mtu mwingine anatumia akaunti yako ya WhatsApp, unapaswa kuwajulisha ndugu na marafiki kwa sababu mtu huyo anaweza kujifanya kuwa wewe katika soga na vikundi. Tafadhali kumbuka, WhatsApp imefumbwa mwisho hadi mwisho na ujumbe huhifadhiwa kwenye kifaa chako, kwa hivyo mtu anayefikia akaunti yako kwenye kifaa kingine hawezi kusoma mazungumzo ya zamani.
Jinsi ya kurejesha akaunti yako
Ingia kwenye WhatsApp ukitumia nambari yako ya simu kisha uthibitishe nambari yako ya simu kwa kuweka msimbo wa tarakimu 6 uliopokea kupitia SMS. Pata maelezo zaidi kuhusu kuthibitisha nambari yako ya simu kwenye Kituo chetu cha Msaada: Android | iPhone.
Mara tu ukiweka msimbo wa tarakimu 6 uliopokea kupitia SMS, mtu anayetumia akaunti yako ataondolewa kiotomatiki.
Huenda pia ukaombwa uweke msimbo wa uhakiki wa hatua mbili. Kama hujui msimbo huu, mtu anayetumia akaunti yako anaweza kuwa aliwasha uhakiki wa hatua mbili. Ni lazima usubiri siku 7 kabla ya kuingia bila msimbo wa uhakiki wa hatua mbili. Bila kujali kama unajua msimbo huu wa kuthibitisha au la, mtu huyo mwingine ametolewa kwenye akaunti mara tu ulipoweka msimbo wa tarakimu 6 uliopokea kupitia SMS. Pata maelezo zaidi kuhusu uhakiki wa hatua mbili kwenye makala haya.
Kumbuka
  • Kama unaweza kufikia akaunti yako na unahisi kuwa mtu anatumia akaunti yako kupitia WhatsApp Web/Desktop, tunakushauri utoke kwenye kompyuta zote ukitumia simu yako.
  • Ili kulinda akaunti yako, WhatsApp itakuarifu wakati mtu anajaribu kusajili akaunti ya WhatsApp kwa nambari yako ya simu. Pata maelezo zaidi kwenye makala haya.
Rasilimali
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La