Akaunti zilizoibiwa

Kuhusu akaunti zilizoibiwa
Usishiriki msimbo wako wa uthibitishaji wa WhatsApp kupitia SMS na wengine, hata kama ni ndugu au marafiki. Ikiwa umehadaiwa ukashiriki msimbo wako na ukapoteza ufikiaji kwenye akaunti yako ya WhatsApp, soma maagizo yaliyo hapa chini ili urejeshe akaunti yako.
Ikiwa unashuku kuwa mtu mwingine anatumia akaunti yako ya WhatsApp, unapaswa kuwajulisha ndugu na marafiki kwa sababu mtu huyo anaweza kujifanya kuwa wewe kwenye soga ya binafsi na ya vikundi. Tafadhali kumbuka, WhatsApp imefumbwa mwisho hadi mwisho na ujumbe huhifadhiwa kwenye kifaa chako, kwa hivyo mtu anayefikia akaunti yako kwenye kifaa kingine hawezi kusoma mazungumzo yako ya zamani.
Jinsi ya kurejesha akaunti yako
Ingia kwenye akaunti ya WhatsApp ukitumia namba yako ya simu kisha uthibitishe namba yako ya simu kwa kuweka msimbo wenye tarakimu 6 utakaopokea kupitia SMS. Pata maelezo zaidi kuhusu uthibitishaji wa namba yako ya simu kwenye Kituo chetu cha Msaada: Android | iPhone.
Mara tu ukiweka msimbo wenye tarakimu 6 utakaoupokea kupitia SMS, mtu anayetumia akaunti yako ataondolewa kiotomatiki.
Huenda pia ukaombwa uweke msimbo wa uthibitishaji wa hatua mbili. Ikiwa hujui msimbo huo, mtu anayetumia akaunti yako anaweza kuwa amewasha uthibitishaji wa hatua mbili. Ni lazima usubiri siku 7 kabla ya kuingia kwenye akaunti bila msimbo wa uthibitishaji wa hatua mbili. Bila kujali ikiwa unajua msimbo huo wa uthibitishaji au la, mtu huyo mwingine ataondolewa kwenye akaunti mara tu utakapoweka msimbo wenye tarakimu 6 utakaoupokea kupitia SMS. Pata maelezo zaidi kuhusu uthibitishaji wa hatua mbili kwenye makala haya.
Kumbuka: Wakati mwingine, WhatsApp inaweza kuthibitisha namba yako ya simu kiotomatiki. Fahamu zaidi.
Kumbuka
  • Ikiwa unaweza kufikia akaunti yako na unashuku kuwa kuna mtu anayetumia akaunti yako kupitia WhatsApp Web au Desktop, tunashauri uondoke kwenye kompyuta zote ukitumia simu yako.
  • Ili kulinda akaunti yako, WhatsApp itakuarifu wakati mtu anajaribu kusajili akaunti ya WhatsApp akitumia namba yako ya simu. Pata maelezo zaidi kwenye makala haya.
Rasilimali
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La