Jinsi ya kukagua msimbo wa QR ya biashara ya WhatsApp

Android
iPhone
Unaweza kuungana na biashara kwenye WhatsApp kwa urahisi kwa kukagua msimbo yao wa QR ya WhatsApp. Kamera ya WhatsApp inaweza tu kukagua misimbo rasmi ya QR ya WhatsApp.
Kagua msimbo wa QR wa biashara
Kagua kwa kibinafsi
 1. Fungua WhatsApp > Mipangilio.
 2. Gusa aikoni ya QR inayoonyeshwa karibu na jina lako.
 3. Gusa Kagua > SAWA.
 4. Shikilia kifaa chako juu ya msimbo wa QR kukagua.
 5. Gusa Endelea kupiga soga.
Unaweza pia kukagua kwa kamera ya WhatsApp:
 1. Fungua WhatsApp > gusa Kamera.
 2. Shikilia kifaa chako juu ya msimbo wa QR kukagua.
Kwenye iPhone 6s au mpya, unaweza kugusa na kushikilia aikoni ya WhatsApp kwenye skrini ya nyumbani kutazama menyu ya haraka. Kisha, gusa Kamera kufungua kamera ya WhatsApp.
Kagua kutoka kwa Picha
 1. Fungua WhatsApp > Mipangilio.
 2. Gusa aikoni ya QR inayoonyeshwa karibu na jina lako.
 3. Gusa Kagua, kisha gusa aikoni Picha iliyopo chini ya skrini.
 4. Chagua picha yenye msimbo wa QR ya WhatsApp kuikagua.
Kukagua kutoka kwa kamera ya WhatsApp
 1. Fungua WhatsApp > gusa Kamera.
 2. Gusa aikoni ya Picha iliyopo chini ya skrini.
 3. Chagua picha yenye msimbo wa QR ya WhatsApp kuikagua.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La