Jinsi ya kushirikisha bidhaa au huduma kutoka kwa orodha

Unaweza kwa urahisi kushirikisha bidhaa na huduma za biashara na marafiki zako.
Shirikisha bidhaa au huduma kutoka kwenye soga ya kibinafsi au soga ya kikundi
 1. Gusa ikoni ya Sambaza iliyo karibu na picha ya bidhaa au huduma.
 2. Tafuta au chagua soga za vikundi au kibinafsi unazotaka kushirikishia bidhaa au huduma.
 3. Gusa Sambaza.
Shirikisha bidhaa au huduma kutoka kwa orodha yako
 1. Nenda kwenye jalada la WhatsApp Business.
 2. Gusa ONA YOTE karibu na ORODHA.
 3. Gusa bidhaa au huduma kutazama Maelezo.
 4. Gusa Zaidi
  > Tuma.
 5. Tafuta au chagua soga za vikundi au kibinafsi unazotaka kushirikishia bidhaa au huduma.
 6. Gusa Tuma.
Shirikisha bidhaa au huduma kutoka kwa orodha kwenye WhatsApp Web au Desktop
 1. Nenda kwenye jalada la WhatsApp Business.
 2. Gusa ONA YOTE karibu na Orodha.
 3. Gusa bidhaa au huduma kutazama Maelezo.
 4. Gusa ikoni ya kunjuzi iliyo juu.
 5. Gusa Tuma Bidhaa
 6. Tafuta au chagua soga ya kibinafsi au za vikundi unazotaka kushirikishia bidhaa au huduma.
 7. Gusa ikoni ya Tuma.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La