Imeshindwa kupakua au kutuma faili za maudhui

Android
Ikiwa unakumbana na hitilafu unapopakua au kutuma picha, video au ujumbe wa sauti, hakikisha yafuatayo:
  • Simu yako ina muunganisho wa intaneti unaofanya kazi wenye mawimbi thabiti. Jaribu kupakia ukurasa wa wavuti ili uhakikishe.
  • Umeweka kwa usahihi kipengele cha tarehe na saa kwenye simu yako. Ikiwa tarehe yako si sahihi, hutaweza kuunganishwa kwenye seva za WhatsApp ili kupakua maudhui yako. Pata maelezo ya jinsi ya kuweka mipangilio yako ya tarehe kwa usahihi hapa.
Tatizo likiendelea, huenda kuna hitilafu kwenye kadi yako ya SD. Ili kuthibitisha, hakikisha kadi yako ya SD ina:
  • Nafasi ya kutosha ya hifadhi. Ikiwa kuna nafasi ya kutosha kwenye kadi ya SD, lakini bado huwezi kupakua faili zozote kwenye kadi hiyo kutoka WhatsApp, huenda ukahitaji kufuta data ya WhatsApp kwenye kadi yako ya SD.
  • Hali ya kusoma tu imezimwa.
Ikiwa hakuna suluhisho lolote lililotatua tatizo hilo, inamaanisha kuwa kadi yako ya SD imeharibika. Katika hali hii, huenda ukahitaji kuandaa upya kadi yako ya SD au kununua kadi mpya ya SD.
Kumbuka: Kuandaa upya kadi ya SD kutafuta maudhui yote ya kwenye kadi ya SD.
Ikiwa bado unakumbana na hitilafu baada ya kujaribu hatua zote zilizoorodheshwa, tafadhali fanya yafuatayo:
  • Thibitisha kuwa unatumia toleo jipya la WhatsApp au usasishe ikihitajika. Pata maelezo ya jinsi ya kusasisha WhatsApp kwenye makala haya.
  • Ikiwa toleo lako la WhatsApp ni sahihi, zima kisha uwashe kifaa chako.
  • Ikiwa kitendo cha kuzima na kuwasha simu yako hakijatatua tatizo, thibitisha kuwa simu yako inatumia toleo jipya la mfumo wa uendeshaji, au usakinishe sasisho ikihitajika.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La